Kila binadamu anastahili kuvuta hewa safi, biashara ya hewa ya ukaa bado changamoto: Tanzania

Kusikiliza /

Dr. Trezya Luoga-Huviza

Lengo namba saba la maendeleo ya Milenia linahusika na uhifadhi wa mazingira ili dunia iweze kuwa mustakhbali endelevu lakini bado inaelezwa kuwa uzalishaji wa hewa chafuzi unaendelea kutishia siyo tu uhai wa binadamu bali pia dunia yenyewe na binadamu hatokuwa na pakukimbilia.

Na hivyo katika mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaoanza hii leo hapa New York, Tanzania ikiwa ni moja ya nchi wanachama inataka kusisitiza umuhimu wa nchi zilizoendelea kupunguza na hatimaye kuacha kuzalisha hewa chafuzi huku ikisema umaskini kwa nchi maskini ndio kikwazo cha uhifadhi wa mazingira. Terezia Luoga-Huviza ni Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais akisimamia Mazingira.

(Sauti ya Waziri Huviza-1)

Mojawapo ya mikakati ya udhibiti wa mazingira ni biashara ya ukaa yaani Carbon trade lakini Waziri Huviza anasema bado safari ni ndefu lakini jitihada zaidi zahitajika.

(Sauti ya Waziri Huviza-2)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930