Idadi ya watu walioathirika na mafuriko Yemen imefikia 50,000:OCHA

Kusikiliza /

Mafuriko Yemen

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA limesema ni mwezi mmoja tangu mvua kubwa na mafuriko kuzikumba wilaya 26 katika majimbo 9 nchini Yemen.

Idadi ya walioathirika imefikia 50,000 huku mvua na mafuriko ikiendelea kuathiri mikoa ya Kusini na Kati mwa nchi hiyo. Kwa mujibu wa OCHA taarifa zaidi za waliopoteza maisha, uharibifu, idadi ya waathirika na juhudi za kukabiliana na hali hiyo zinazidi kujitokeza.

Mvua kubwa zilizonyesha Septemba 9 zilisababisha mafuriko makubwa kwenye wilaya za Hufash, Milhan na Al Khabt kwenye jimbo la Al Mahwit , wanawake wawili walizama, mashamba kusombwa, barabara zimebomoka na visima 14 vya maji kuharibiwa. OCHA inasema familia 30 zimechukua hifadhi kwenye shule wilayani Ta’iziyah baada ya mafuriko kubomoa nyumba zao,na kuharibu kila kitu.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031