Harakati mpya za Katibu Mkuu kuhusu mzozo wa Syria, Brahimi aelekea G-20

Kusikiliza /

Lakhdar Brahimi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema mwakilishi wa pamoja wa Umoja huo na nchi za kiarabu katika suala la Syria Lakhdar Brahimi anaelekea Urusi kuangalia jinsi ya kuweka ushawishi mpya ili mkutano wa pili kuhusu Syria uweze kufanyika.

Amesema wakati huu ambapo dunia inajikita juu ya hofu ya matumizi ya silaha za kemikali huko Syria, Brahimi atamsaidia huko St. Petersburg kushinikiza kufanyika kwa mkutano huo wa Geneva. Amesema suluhu la kisiasa ndio njia pekee ya kumaliza umwagaji damu nchini Syria.

(SAUTI YA BAN)

"Wakati viongozi wanashiriki mkutano wa G20 kujadili hali ya uchumi wa dunia, hali ya sasa inayochochewa na tuhuma za matumizi ya silaha za kemikali na kuzorota kwa hali ya kibinadmu huko Syria,udharura utahitajika kwa viongozi wa dunia kusaka utashi wa kisiasa kushughulikia suala hili, ndio maana nimemuomba Brahimi aungane nami hapa St. Petersburg  ili kushinikiza kufanyika kwa mkutano wa pili wa Geneva kuhusu Syria."

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930