Hali ya kibinadamu ya zaidi ya watu 150,000 Ufilipino inatia hofu: OCHA

Kusikiliza /

Ofisi ya kuratibu misaada ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, OCHA imeelezea wasiwasi wake kuhusu hali ya kibinadamu ya takriban watu 158,000 ambao wameathiriwa na mapigano kati ya kundi la wanamgambo wa Moro National Liberation Front na wanajeshi wa serikali katika mji wa Zamboanga na Mkoa wa Basilan Kusini mwa Ufilipino.

Tangu Septemba 9, watu wapatao 130,000 wamelazimika kuhama kufuatia mapigano hayo ambayo yanaendelea. Makazi ya zaidi ya familia laki moja yameharibiwa kabisa, huku vituo vya afya na shule pia zikiharibiwa.

Kulingana na takwimu za serikali, takriban watu laki moja wamewwekwa katika vituo 33 vya dharura, vikiwemo shule 16.

Umoja wa Mataifa na wadau wasio wa kiserikali wamefanya tathmini ya haraka ya mahitaji katika vituo hivyo vya dharura vya uokozi mnamo Septemba 18, na kutambua kuwa vituo vingi havina mahema na maji ya kutosha, hku pia vikikosa huduma za usafi. Watu walolazimika kuhama wanahitaji kwa dharura huduma za afya, zikiwemo chanjo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29