Hali ya chakula nchini Zimbabwe yazidi kuzorota: WFP

Kusikiliza /

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP linasema zaidi ya watu Milioni Mbili nchini Zimbabwe wanakabiliwa na uhaba wa chakula. Grace Kaneiya na ripoti kamili.

(Taarifa ya Grace)

Katika kukabiliana na hali hiyo ya uhaba wa chakula Zimbambwe, WFP na washirika wake watagawa nafaka pamoja na mafuta ya kupikia. Pia mgao wa fedha utatolewa kwenye maeneo fulani kama moja ya njia ya kuhakikisha kuendelea kuhudumu kwa masoko. Huduma hiyo inatarajiwa kuendeshwa kuanzia mwezi Oktoba mwaka huu hadi msimu wa mavuno mwezi Machi mwaka ujao. Elisabeth Byrs ni msemaji wa WFP.

(SAUTI YA ELIZABETH BYRS)

“Hali ya usalama wa chakula inadorora na ni mbaya zaidi kuwahi kushudiwa tangu 2009. Kukosekana kwa usalama wa chakula nchini Zimbabwe kumesababishwa na mambo kadha ikiwemo, hali ya hewa, kupanda kwa gharama ya maisha, na kukosekana kwa mbolea na mbegu na uwezekano wa ongezeko la bei za vyakula kwa sababu ya mavuno duni. Tunashirikiana na serikali kuimarisha ustahimili wa jamii, na kwa sasa tunasubiri msimu wa mavuno ni lazima tuwapatie msaada wa chakula”

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2017
T N T K J M P
« jul    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031