Falk akaribisha uamuzi wa Uholanzi kujiondoa katika mradi haramu wa maji Israeli

Kusikiliza /

Richard Falk

Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya kibinadamu  Richard Falk leo amekaribisha uamuzi uliotolewa na kampuni ya kimataifa ya Kiholanzi Royal HaskoningDHV kusitisha mkataba wake na manispaa ya Jerusalem wa kujenga kiwanda cha maji machafu Kidroni chenye lengo la kuhudumia makazi haramu ya Israeli katika Mashariki ya Jerusalemu.

Kukamilika kwa mradi huo kungetoa fursa zaidi kwa wahamiaji haramu wa Israeli kupenyeza katika eneo la Mashariki mwa mji wa Jerusalem hatua ambayo inaelezwa ni uvunjifu wa azimio la Umoja wa Mataifa.

Mtaalamu huyo wa Umoja wa Mataifa amepongeza hatua  iliyochukuliwa na kampuni hiyo iliyoamua kusitisha ujenzi wa mradi huo ambao ungezidisha hali ya uhasama.

Amesema kuwa ametiwa moyo na namna baadhi ya mashirika yanavyowajibika kuheshimu na kutekeleza kwa vitendo sheria za kimataifa

Katika taarifa yake, Kampuni hiyo ya Holland, hatua ya kusitishwa ujenzi huo imechukuliwa baada ya majadiliano marefu baadhi ya wadau na kubaini kuwa kujuhusisha kwake kwenye mradi huo kungekuwa ni kwenda kinyume na sheria za kimataifa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031