Chad yapongezwa kwa juhudi za mchango wa amani Afrika:

Kusikiliza /

Rais Idriss Deby wa Chad

Rais wa Chad Idriss Deby Itno amekutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon kandoni mwa mjadala wa baraza kuu la 68.

Bam ameipongeza serikali ya Chad kwa juhudi za mchango wake katika kuleta amani barani Afrika na hasa kwa kuchangia vikosi hivi karibuni kwenda kulinda amani nchini Mali.

Viongozi hao wawili pia wamejadili hali ya Chad hususani ongezeko la wakimbizi na wakimbizi wa ndani.Ban na Rais Deby wamebadilishana mawazo pia kuhusu hali katika nchi jirani ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na kusisitiza uharaka wa kurejesha amani , kuongeza msaada wa kimataifa katika utawala wa mpito na kushughulikia mahitaji ya kibinadamu.

Katibu Mkuu pia amethibitisha nia ya Umoja wa Mataifa kuisaidia Chad katika uchaguzi mkuu ujao.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2017
T N T K J M P
« sep    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031