Bila uongozi wa kisheria hakuna usalama wala uwajibikaji: Ban

Kusikiliza /

Bila uongozi wa kisheria, hakuwezi kuwa na usalama au uwajibikaji, na ukiukwaji wa haki za binadamu hutendeka bila kukabiliwa kisheria. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon wakati akipokea tuzo ya Uongozi wa Kisheria ya LexisNexis jana jioni kwa niaba ya UM. Tuzo hiyo imetolewa na mashirika mawili: lile la LexisNexis ambalo linajishulisha na kupiga vita usafirishaji haramu wa watu na Atlantic Council ambalo huendeleza usalama wa kimataifa. Bwana Ban ameyasifu mashirika hayo hayo kwa kazi yanayofanya. Amesema ukosefu wa sheria huzaa manung’uniko na ghasia na migogoro. Ameongeza kuwa ukosefu wa usalama huzuia ukuaji wa kiuchumi na maendeleo endelevu. Katibu Mkuu amesema jamii zisizokuwa na mfumo wa kisheria unaotegemewa ni jamii ambako watu hawawekezi katika siku zao zijazo au katika mustakabali wa nchi yao. Bwana Ban amesema Umoja wa Mataifa unashirikiana na wote ambao wana hamu ya kujenga uongozi thabiti wa kisheria.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2017
T N T K J M P
« jul    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031