Bei za kimataifa za chakula zazidi kushuka:FAO

Kusikiliza /

Muuzaji chakula

Bei za chakula zimeshuka kwa mwezi wa nne mfululizo na mwezi Agost kufikia bei za chini kabisa tangu mwezi Juni mwaka 2012 limesema shirika la chakula na kilimo FAO.

Orodha ya bei ya FAO inapima viwango vya mabadiliko ya bei ya kila mwezi katika bidhaa za chakula kimataifa. Na Kwa mwezo Agost point ni 201.8 karibu point 4 pungufu ya ilivyokuwa Julai na point 11 chini ya mwezi Agost 2012.

FAO inasema kushuka kwa bei mwezi uliopita ni kulisababishwa na kuendelea kuporomoka kwa bei za kimataifa za nafaka na mafuta. Kwa mujibu wa FAO kumekuwa na anguko kubwa la bei ya nafaka mwaka huu.

FAO pia inasema uzalishaji wa nafaka, mpunga na mahidi unatarajiwa kuongezeka 2013. Hata hivyo bei za bidhaa za maziwa, nyama na sukari zimeongezeka kidogo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031