Baraza la usalama lapitisha azimio kuhusu silaha za kemikali Syria.

Baraza la usalama

Baraza la usalama usiku huu limekutana na kupitisha kwa kauli moja azimio kuhusu silaha za kemikali Syria. Azimio hilo linafuatia mashauriano ya awali ya rasimu hiyo jana usiku na linajumuisha viambatanisho viwili, cha kwanza kikiwa ni taratibu za kuteketeza silaha hizo kilichoandaliwa na Baraza tendaji la shirika la kimataifa la kutokomeza usambazaji wa silaha za kemikali, OPCW na taarifa ya pamoja ya makubaliano ya mkutano wa kimataifa wa Syria yaliyopitishwa Geneva mwezi Juni mwaka jana. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon alikuwepo katika kikao hicho na kusema kuwa ni hatua ya kihistoria na baraza limezungumza.

 

(Sauti ya Ban)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930