Ban na Malkia Sofia wa Hispania wazungumzia masuala ya ulemavu na Syria

Kusikiliza /

Katibu Mkuu Ban Ki-moon na Malkia Sophia wa Hispania

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amekuwa na mazungumzo na Malkia Sofia wa Hispania mjini New York, ambako amekuja kwa ajili ya kupokea tuzo maalum ya nchi yake kuhusu harakati za kusaidia watu wenye ulemavu. Katika mazungumzo yao wamejadili mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu ulemavu na maendeleo utakaofanyika tarehe 23 mwezi huu. Bwana Ban na Malkia Sofia wametilia mkazo umuhimu wa kuendeleza haki za binadamu za watu wanaoishi na ulemavu. Hata hivyo Katibu Mkuu amesifu hatua za Malkia Sofia za kusaidia huduma za maji safi, haki za binadamu na utekelezaji aw malengo ya maendeleo ya Milenia duniani kote sambamba na mchango wake wa kuandaa ajenda ya maendeleo baada ya ukomo wa malengo ya milenia. Halikadhalika wamezungumzia Syria na hatua za Umoja wa Mataifa za kushughulikia suala hilo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930