Ban asifu maafikiano kati ya Urusi na Marekani kuhusu silaha za kemikali za Syria

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amekaribisha taarifa ya kwamba waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry na yule wa Urusi Sergei Lavrov wamefikia makubaliano huko Geneva juu ya uhifadhi salama na uteketezaji wa silaha za kemikali za Syria. Taarifa kutoka msemaji wa Umoja wa Mataifa imemkariri Bwana Ban akisema ana matarajio ya kufahamu zaidi juu ya maafakiano hayo na ameahidi kuwa ofisi yake itatoa usaidizi katika utekelezaji. Bwana Ban ameelezea ni marumaini yake ya dhati kuwa makubaliano hayo kwanza kabisa yatazuia matumizi ya baadaye ya silaha za kemikali na kusaidia kupatikana kwa suluhu la kisiasa na hatimaye kumaliza machungu yanayowapata wananchi wa Syria. Wakati huo huo, Katibu Mkuu amepokea rasmi nyaraka za Syria za kujiunga na mkataba wa kutokomeza silaha za kemikali. kwa mujibu wa taratibu Syria itakuwa mwanachama rasmi kuanzia tarehe 14 mwezi ujao.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2017
T N T K J M P
« ago    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
252627282930