Ban aongea kwa simu na mkuu wa tume ya uchunguzi wa silaha za kemikali Syria Dr. Åke Sellström:

Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa leo Jumapili amezungumza kwa njia ya simu na Dr. Åke Sellström, mkuu wa tume mya Umoja wa mataifa ya uchunguzi wa madai ya matumizi ya silaha za kemikali nchiniSyria.

Dr. Sellström, ambaye ndio amerejea tuu The Hague na wataalamu wengine wa tume baada ya kufanya uchunguzi tangu Agost 19 hadi 31 Syria , amempa taarifa Katibu Mkuu za hatua zitakazofuata kwenye mchakato wa uchunguzi.

Amemwambia kuwa matayarisho yote ya kutanabaisha sampuli yanaendelea vyema na sampuli zitaanza kupelekwa maabara kesho Jumatatu.

Dr. Sellström amemwambia Katibu Mkuu kwamba maafisa wawili waSyriawanaangalia mchakato mzima, na kwamba mchakato wote utafanyika kwa kuzingatia viwango vya hali ya juu vya utambuzi vilivyowekwa na shirika linalopinga silaa za nyuklia.

Katibu Mkuu amemtaka Dr. Sellström kuharakisha uchambuzi wa sampuli na taarifa zilizokusanywa na tume yake bila kuathiri muda wa kisayansi wa kupata majibu sahihi na kisha kuripoti kuhusu matokeo ya sampuli hizo haraka iwezekanavyo kwake. Watu hao wawili pia wamejadili njia za kuharakisha mchakato mzima.

Mwisho Ban amemshukuru Dr. Sellström kwa jukumu alilochukua pamoja na timu nzima wakiwaSyrialicha ya changamoto na mazingira magumu waliyokabiliana nayo.

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2016
T N T K J M P
« apr    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031