Ban akutana na Wazriri wa Mambo ya Nje wa Iraq

Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq, Hoshyar Zebari. Katika mazungumzo hayo, Bwana Ban amempa maelezo waziri huyo kuhusu juhudi za hivi karibuni zaidi kwa ajili ya Syria, kufuatia azimio la Baraza la Usalama jana usiku.

Katibu Mkuu ameishukuru Iraq kwa ukarimu wake wa hivi sasa kwa wakimbizi wa Syria, na wote wawili kuelezea haja ya kuwepo rasilmali zaidi ili kuisaidia Iraq kukidhi mahitaji ya kibinadamu ya wakimbizi hao.

Bwana Ban ameelezea wasiwasi wake kuhusu mzozo wa kisiasa na hali ya usalama inayoendelea kuzorota nchini Iraq, na kurejelea wito wake kwa viongozi wa Iraq waendeleze mazungumzo ya amani na kasi ya maridhiano. Ameisihi serikali ya Iraq pia ihitimishe uchunguzi katika matukio ya mauaji ya Septemba 1 kwenye kambi ya Camp Iraq na kuwawajibisha wahusika kisheria.

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031