Ban akutana na mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa yenye wajumbe wa kudumu katika baraza la usalama

Kusikiliza /

Bendera za nchi zenye wajumbe wa kudumu katika baraza la usalama

Hii leo mjini New York, kando mwa mikutano ya baraza kuu la Umoja wa Mataifa, Katibu Mkuu Ban Ki-Moon amekuwa na mazungumzo na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi tano wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama ambazo ni China, Urusi, Marekani, Ufaransa na Uingereza.

Mazungumzo hayo wakati wa mlo maalum wa mchana yalijikita zaidi katika Syria na jinsi ya kuandaa chombo cha pamoja kati y a Umoja wa Mataifa na shirika la kimataifa la kudhibiti silaha za kemikali, OPCW kwa lengo la kukagua na kuhifadhi silaha za kemikail za Syria. Viongozi hao wamebadilishana mawazo kuhusu muda wa kufanyika hilo na masuala mengine yanayohusiana na mkutano wa kimataifa wa amani ya Syria huko Geneva. Wamesisitiza umuhimu wa kuharakisha jitihada za kupatia suluhu mkwamo wa misaada ya kibinadamu kwa wasyria walio nchini mwao na wale walio nchi jirani.

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031