Ban akutana na Marais wa Malawi na Namibia:

Kusikiliza /

Katibu Mkuu Ban akutana na rais Hilde wa Malawi na rais Hifikepunye wa Namibia

Rais wa Malawi Bi Joyce Hilda Mtila Banda ambaye pia ndiye mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya maendeleo kwa nchi za Kusini mwa Afrika SADC pamoja na Rais wa Namibia Bwana Hifikepunye Pohamba wamekutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon hapa New York kando ya mjadala wa baraza kuu.

Katika mkutano wao Ban amekaribisha mchango muhimu wa SADC katika kusaka amani na utulivu kwenye eneo la maziwa makuu, na pia msaada wake katika amani , usalama na mpango wa ushirikiano.

Ameongeza kuwa mchango wao pia katika mazungumzo ya Uganda baiana ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kundi la M23.

Ban ameishukuru pia SADC kwa jukumu lake nchini Madagascar na kwa kuunga mkono kazi za Umoja wa Mataifa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031