Afghanistan iko katika kipindi muhimu sana:Pillay

Kusikiliza /

Navi Pillay

Afghanistan iko katika kipindi muhimu sana hasa katika mabadiliko yanayoendelea ya kisiasa, kiusalama na kiuchumi ambayo yanatarajiwa kukamilika mwaka 2014. Akizungumza na waandishi wa habari Jumanne kamisha mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay amesema mabadiiliko yote hayo yatakuwa na athari katika haki za binadamu za wananchi.

Ameongeza kuwa ukatili dhidi ya wanawake bado ni tatizo na kusema kwamba mafanikio yaliyopatikana katika miaka 12 iliyopita hayawezi kuwa sadaka ya kisiasa katika miezi hii michache kabla ya uchaguzi.

Amesema Afghanistan inapaswa kuhakikisha kwamba mabadiliko yanayotokea kabla ya mwisho wa mwaka 2014 hayatochagiza kuzorota kwa haki za binadamu kwa watu na hususani kwa wanawake. Bi Pillay amesema taifa hilo limeteseka vya kutosha katika miaka 34 ya vita, uharibifu, ukimbizi, njaa, chuki na kunyimwa haki.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031