Nyumbani » 27/09/2013 Entries posted on “Septemba 27th, 2013”

Baraza la Usalama limeweka historia: Ban awaeleza waandishi wa habari

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon

Ni siku ya kihistoria, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon aliwaeleza waandishi wa habari punde baada ya baraza la usalama kupitisha azimio kuhusu uteketezaji wa silaha za kemikali zaSyria. Hata hivyo amesema kuteketeza silaha za kemikali kwenye nchi iliyo katika vita vya wenyewe kwa wenyewe ni kazi kubwa lakini wanashirikiana na OPCW kuandaa [...]

27/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wajumbe wa Baraza la Usalama wapitisha mswada wa Syria:

Kusikiliza / Upigaji kura SC

Wajumbe wa kudumu wa baraza la usalama na wale wasio wa kudumu Ijumaa jioni wamepiga kura ya mswaada wa azimio kuhusu silaha za kemikali nchini Syria. (SAUTI YA RAIS WA BARAZA)  Akizungumzia azimio hilo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kwa mujibu wa uchunguzi wa tume ya Umoja wa Mataifa ya uchunguzi [...]

27/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la usalama lapitisha azimio kuhusu silaha za kemikali Syria.

Baraa la usalama

Baraza la usalama usiku huu limekutana na kupitisha kwa kauli moja azimio kuhusu silaha za kemikali Syria. Azimio hilo linafuatia mashauriano ya awali ya rasimu hiyo jana usiku na linajumuisha viambatanisho viwili, cha kwanza kikiwa ni taratibu za kuteketeza silaha hizo kilichoandaliwa na Baraza tendaji la shirika la kimataifa la kutokomeza usambazaji wa silaha za [...]

27/09/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban na waziri wa mambo ya nje wa Urusi wajadili suluhu ya mgogoro wa Syria

Kusikiliza / Ban Ki-moon na Sergey V. Lavrov

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon jioni ya leo Ijumaa amekutana na waziri wa mambo ya nje wa shirikisho la Urusi Sergey V. Lavrov. Viongozi hao wawili wamejadili masuala mbalimbali Katibu Mkuu Ban amesisitiza haja ya kutafuta suluhu ya kisiasa katika mgogoro ambao sasa umekuwa wa muda mrefu wa Syria. Pia amesema ni [...]

27/09/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Quartet yakutana kuzungumzia hatua za majadiliano baina ya Israel na Palestina:

Kusikiliza / Wawakilishi wa QUartet

Wawakilishi wa Quartet ambao ni Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon, waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov, waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry, na mwakilishi wa sera za nje na usalama wa Muungano wa Ulaya Catherine Ashton,wamekutana mjini New York leo kando na mjadala wa baraza kuu [...]

27/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa Baraza Kuu la UM ukishika kasi, Viongozi wa Afrika watathimini malengo ya milenia

Kusikiliza / Makao Makuu ya UM

Tarehe 24 mwezi huu wa Septemba mkutano wa 68 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ulianza rasmi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani. Wakuu wa nchi, marais na mawaziri kutoka nchi 193 wanachama wa umoja huo wanashiriki katika mjadala huo utakaomalizika tarehe Pili mwezi ujao. Je Afrika Mashariki ilikuja [...]

27/09/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Tanzania yajivunia kutimiza malengo 4 kati ya 8 ya milenia:Kikwete

Kusikiliza / Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania akihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete amesema Tanzania inajivunia kutanabaisha kwamba malengo manne kati ya manane ya maendeleo ya Milenia yametimizwa. Akizungumza katika mjadala mkuu wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa Ijumaa jioni amesema… (SAUTI YA KIWETE) Ameongeza kuwa kuna haja ya kuendeleza utekelezaji wa kutimiza malengo hayo hata baada [...]

27/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hata baada ya 2015 tuna wajibu wa kutimiza malengo yaliyosalia:Mwinyi

Kusikiliza / Dr Hussein Mwinyi

Waziri wa afya wa Tanzania Dr Hussein Mwinyi amesema pamoja na serikali ya Tanzania kutimiza lengo la nne la milenia ambalo ni kupunguza vifo vya watoto wa chini ya miaka mitano, taifa hilo bado lina wajibu wa kuhakikisha malengo mengine yaliyosalia yanatimizwa hata baada ya ukomo wa malengo hayo mwaka 2015. Akizungumza na Idhaa ya [...]

27/09/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Suala la tindikali laibuka kwenye mazungumzo kati ya Ban na Rais Kikwete

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon na Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amekuwa na mazungumzo na Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania ambapo ametoa shukrani kwa mchango wa nchi hiyo kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko DRC, MONUSCO na kule Darfur, UNAMID. Katikahilo, viongozi hao wawili wameelezea masikitikoyaokufuatia vifo vya walinda amani waTanzaniana wamejadili uwezo wa kikosi cha kujibu [...]

27/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban asikitishwa na ripoti mpya kuhusu mabadiliko ya tabianchi

Kusikiliza / Katibu Mkuu, Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon, amekaribisha ripoti ya tathmini ya tano ya jopo la kiserikali kuhusu mabadiliko ya tabianchi, IPCC na kusikitishwa na matokeo yake. Ripoti hiyo inaweka dhahiri kuwa madhara anayosababisha mwanadamu kwenye mfumo wa tabianchi ni bayana katika maeneo mengi ya dunia, na inawezekana kuwa madhara hayo alosababisha mwanadamu yamekuwa [...]

27/09/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Juhudi zaidi zahitajika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa:Figures

Kusikiliza / Cristiana Figueres

Katibu Mkuu wa Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya hali ya hewa UNFCCC Christiana Figures na maafisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa wamesema matokeo ya utafiti wa karibuni wa ripoti ya IPCC kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa ni wito wa wazi kwa jumuiya [...]

27/09/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Angola yamulika amani DRC, yataka marekebisho ya muundo wa Baraza la Usalama

Kusikiliza / Manuel Domingos Vicente

Suala la amani ya kudumu Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ni miongoni mwa mambo yaliyokuwemo kwenye hotuba ya Makamu wa Rais wa Angola Manuel Domingos Vicente aliyotoa kwenye baraza kuu la Umoja wa Mataifa kwa niaba ya Rais wa Angola Jose Eduardo Dos Santos. Bwana Vicente amesema hali eneo hilo linatishia usalama [...]

27/09/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

IOM imepokea dola milioni 2 kuwasaidia Wahaiti walio makambini, yakarabati nyumba za waliopoteza makazi Syria.

Kusikiliza / Msemaji wa IOM Jumbe Omari Jumbe

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limesema limepokea dola milioni mbili kutoka serikali ya Sweden kama mchango wa kuwalinda wananchi zaidi ya laki mbili walioathirika kufuatia tetemeko la ardhi mwezi Januari mwaka  2010 nchini Haiti Msemaji wa IOM Jumbe Omari Jumbe anafafanua namna msaada huo utakavyotumika  (Sauti ya Jumbe) Wakati huo huo shirika hilo la [...]

27/09/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Migogoro nchini Mali inatokana na hali ngumu ya maisha:Rais Keita

Kusikiliza / Rais wa Mali, Ibrahim Boubakar Keita

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambapo katika siku ya nne hii leo viongozi wameendelea kuhutubia wakijikita katika masuala ya ulinzi, amani usalama na maendeleo. Grace Kaneiya na ripoti kamili. (Taarifa ya Grace) Akitoa hotuba yake wakati wa mjadala mkuu wa Baraza Kuu, Rais mpya wa Mali Ibrahim Boubakar Keita amewasilisha shukrani za watu wa [...]

27/09/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kuanza utekelezaji wa mkataba wa kupinga majaribio ya nyuklia ni muhimu:Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM, Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amesema hatua zimepigwa tangu mkutano wa mwaka 2011 wa kuhusu kuanza kutekelezwa kwa mkataba wa kupinga majaribio ya nyuklia. Amesema nchi tano mpya zimejiunga katika mkataba huo ili kufanikisha nia ya kimataifa ya kupinga majaribio ya nyuklia. Amezipongeza nchi hizo ambazo ni Brunei, Chad, Guatemala, Guinea-Bissau, Indonesia [...]

27/09/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mawaziri wa muungano wa ustaarabu wakutana kuridhia mkakati mpya wa ushirikiano

Kusikiliza / Nassir Abdulaziz al Nasser

Hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, mkutano wa mawaziri wa nchi marafiki wa Muungano wa Ustaarabu, UNAOC, umefanyika pembezoni mwa mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo.Alice Kariuki ana maelezo zaidi (TAARIFA ya ALICE) Mbali na kupokea maelezo zaidi kuhusu maandalizi ya mkutano ujao wa kimataifa wa muungano huo nchini [...]

27/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Twapongeza jitihada za AU za kuleta maridhiano Sudan na Sudan Kusini: Eliasson

Kusikiliza / Wakati wa mkutano wa Sudan na Sudan Kusini

Mashauriano ya pili ya ngazi ya mawaziri kutoka Sudan na Sudan Kusini yamefanyika hii leo mjini New York, mada kuu ikiwa ni mchakato wa amani wa kumaliza mzozo kati ya nchi mbili hizo. Ripoti ya Assumpta Massoi inafafanua zaidi.  (Taarifa ya Assumpta) Sudan na Sudan Kusini ziliwakilishwa na mawaziri wao wa mambo ya nje ambapo [...]

27/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban asikitishwa na kifo cha mlinda amani wa Tanzania DRC:

Kusikiliza / Walinda amani, MONUSCO

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema amestushwa na kifo cha mlinda amani wa Kitanzania ambaye alijeruhiwa kwenye mapigano Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwisho wa mwezi Agost. Mlinda amani huyo alijeruhiwa wakati wapiganaji wa M23 waliposhambulia eneo la Umoja wa Mataifa karibu na milima ya Kibati Kaskazini mwa Goma. Mlinda amani huyo [...]

27/09/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wachunguzi wa UM wa silaha za kemikali Syria wanafanyia kazi ripoti ya mwisho.

Kusikiliza / Ake Sellstrom, anayeongoza timu ya uchunguzi wa silaha za kemikali Syria

  Tume ya Umoja wa mataifa inayochunguza madai ya matumizi ya silaha za kemikali Syria Ijumaa imeendelea kuifanyia kazi ripoti ya mwisho ambayo inatarajia itakuwa tayari mwishoni mwa mwezi Oktoba. Flora Nducha na ripoti kamili  (RIPOTI YA FLORA NDUCHA) Ripoti hiyo inatokana na madai mbalimbali yaliyowasilishwa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa na saba [...]

27/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yakaribisha uamuzi wa Brazil kutoa viza kwa wakimbizi wa Syria

Kusikiliza / Wahamiaji wa Syria

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR limekaribisha hatua ya kamati ya kitaifa ya Brazil iliyoeleza kusudia lake la kutoa vibali vya kuingia nchini humo au viza kwa raia wa Syria na wan chi nyingine ambao wameathirika na mapigano yanayoendelea.  Kamati hiyo CONARE imesema kuwa iko tayari pia kutoa viza kwa wale wanakusudia kuomba [...]

27/09/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Uganda yapata chuo cha uhamiaji ili kupanbana na uhalifu wa kimataifa

Kusikiliza / Wakati wa uzinduzi wa chuo, Uganda

Katika mapambano dhidi ya uhalifu wa kimataifa ukiwemo ugaidi na usafirishaji haramu wa binadamu, Uganda imeanzisha chuo cha uhamiaji ili kuimarisha usalama kwenye mipaka yake. John Kibego wa radio washirika ya Spice FM Uganda, ana ripoti kamili (Tarifa ya John Kibego) Chuo hiki kimezinduliwa kwenye eneo la chuo cha zamani cha jeshi la wanhewa na [...]

27/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

OCHA yaelezea hofu yake dhidi ya mauaji ya raia Ituri

Kusikiliza / Nembo ya OCHA

Shirika la Umoja wa mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA limeelezea hofu yake juu ya mauaji ya raia 10 wakiwemo wafanyakazi watatu wa afya kwenye eneo la Geti wilaya ya Ituri jimbo la Orientale nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. OCHA inasema mauaji ya raia na mauaji ya aina yoyote [...]

27/09/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031