Nyumbani » 26/09/2013 Entries posted on “Septemba 26th, 2013”

Rasimu ya azimio kuhusu Syria yawasilishwa Baraza la Usalama, kupigiwa kura: Balozi Churkin

Kusikiliza / Balozi Vitaly I. Churkin

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa Alhamisi limekuwa na mashauriano ya faragha kuhusu Syria ambapo Urusi na Marekani ziliwasilisha rasimu ya azimio kwa Syria, kufuatia shambulio la kemikali kwenye eneo la Ghouta, nje kidogo ya mji mkuu wa nchi hiyo, Damascus,tarehe 21 mwezi uliopita. Mwakilishi wa kudumu wa Urusi kwenye Umoja wa Mataifa Balozi [...]

26/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ulimwengu una uwezo na jukumu la kuumaliza mzozo wa Syria: UM

Oscar Toranco

Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zina uwezo na jukumu la kukabiliana na mzozo wa Syria, ambao umetajwa na kuwa changamoto kubwa zaidi kwa amani na usalama ulimwenguni, na kukomesha ukatili ambao raia wa Syria wanaendelea kupitia. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Ban Ki-Moon, katika taarifa ilotolewa na msaidizi wake wa masuala ya kisiasa, Oscar [...]

26/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tunahitaji msaada kuimarisha miundombinu: Sudani Kusini

Kusikiliza / Makamu wa Rais wa Sudan Kusini James Igga

Makamu wa rais wa Sudan Kusini James Igga ni miongoni viongozi waliohutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kusema nchi yake inahitaji msaada mkubwa jumuiya ya kimataifa hususani katika miundombinu baada ya mapigano kuathiri kwa asilimia kubwa njia za usafiri. Katika mahojiano maalum na idhaa hii kandoni mwa mkutano huo Bwana Igga amesema ni [...]

26/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Arobaini ya Al Shabaab kutimia, ICC yatia mashaka:Rais Mohamoud

Kusikiliza / Rais hassanSheikh Mohamoud wa Somalia

Rais Hassan Sheikh Mohamoud wa Somalia ameliambia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuwa uthabiti wa kikundi cha kigaidi nchini Somalia unazidi kuzorota lakini bado jitihada zaidi za kimataifa, kikanda na kitaifa zinahitajika ili kuweza kusambaratisha kabisa kikundi hicho kinachoendelea kuua raia wasio na hatia. Amesema tukio la Kenya hivi karibuni kinadhihirisha kuwa jitihada zaidi [...]

26/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban akutana na kuzungumza na waziri mkuu wa Ethiopia

Kusikiliza / Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kin Moon amekutana na kufanya mazungumzo na waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn ambaye ni mwenyekiti wa umoja wa Afrika AU. Katibu Mkuu ametumia fursa hiyo kumshukuru kiongozi huyo wa Ehtiopia kwa namna nchi yake ilivyowezesha upatanishi huko Jubaland Somalia. Viongozi hao walijadili hatua za kuimarisha amani nchini [...]

26/09/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ujangili wa wanyamapori ni tishio kwa amani na usalama barani Afrika: Rais Bongo

Kusikiliza / Rais wa Gabon Ali Bongo Ondimba

Suala la ujangili wa ndovu na kifaru pamoja na uvunaji haramu wa mazao ya misitu limeangaziwa ndani ya Umoja wa Mataifa hii leo wakati wa kikao cha ngazi ya juu kilichoandaliwa na serikali ya Ujerumani na Gabon. Kubwa lililoibuka ni kutaka Umoja wa Mataifa kuwa na dhima kuu katika kudhibiti matukio hayo kama vile kuwepo [...]

26/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zimbabwe haitakuwa koloni tena, vikwazo viondolewe: Mugabe

Kusikiliza / Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amehutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambapo amegusia masuala ya marekebisho ya muungo wa Umoja wa Mataifa ikiwemo baraza la usalama pamoja na kile alichokiita ni njama za kurejesha ukoloni mamboleno nchini mwake. Rais Mugabe amesema hoja ya Afrika ya kutaka muundo wa Baraza la usalama ufanyiwe na marekebisho [...]

26/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban akaribisha uamuzi wa mahakama ya rufaa kuhusu Sierra Leone kwa kifungo cha Taylor

Kusikiliza / Charles Taylor

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon, amekaribisha uamuzi wa Mahakama ya Rufaa kwa ajili ya Sierra Leone, wa kutupilia mbali ombi la rufaa la rais wa zamani wa nchi hiyo, Charles taylor, la kutaka kifungo chake cha miaka 50 ipinduliwe. Kwa kauli moja, mahakama hiyo maalum ya rufaa iliamua kushikilia makosa yote kumi [...]

26/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban asikitishwa na vifo vya tetemeko la ardhi Pakistan:

Kusikiliza / Pakistan earthquake2

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesem amesikitishwa na maisha ya watu yaliyopotea nchini Pakistan kutokana na tetemeko la ardhi. Tetemeko la ukuwa wa vipimo vya rishta 7.8 lililikumba eneo la Balochistan tarehe 24 Septemba na kusababisha uharibifu mkubwa , huku likibomoa maelfu ya nyumba na kupoteza maisha ya watu. Ban ametuma salamu [...]

26/09/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Uganda yahaha kunusuru mazingira

Kusikiliza / mazingira

Utunzaji wa mazingira ni miongoni mwa malengo manane ya maendeleo ya milenia yanayojadiliwa katika mkutano wa 68 wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa, ili kutathimini utekelezaji wake.   Kufahamu hali ya utunzaji wa mazingira  ilivyo nchiniUgandaungana na John Victor Kibego anayeainisha juhudi za  serikali katika kukemea uharibifu wa mazingira nchini humo  

26/09/2013 | Jamii: Mahojiano, Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

Viongozi wa Afrika wazungumzia ukuaji wa uchumi katika bara lao:

Kusikiliza / Kikao cha 68 cha Baraza Kuu

Wakilaani vita vinavyoendelea Syria na kwingineko viongozi wa dunia ambao wamewasilisha ripoti zao wameelezea na kupongeza ushirikiano baina ya amani na maendeleo katika mjadala wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa ambao leo umeingia siku ya tatu. Rais Joseph Kabila Kabange wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amesema usalama unasalia kuwa kitovu muhimu cha maendeleo [...]

26/09/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Sekta ya mifugo yaweza kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi: FAO

Kusikiliza / Mifugo

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO linasema kuwa kiwango cha utoaji wa gesi joto na zile chafuzi katika sekta ya mifugo kinaweza kupunguzwa kwa asiilmia 30 iwapo wafugaji watatumia njia bora za ufugaji kuanzia utafutaji wa malisho hadi matumizi ya mboji. Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya FAO kama anavyoripoti George Njogopa. [...]

26/09/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Rais Pohamba asifu kazi ya kikosi cha UM cha kulinda amani DRC

Kusikiliza / Rais Hifikepunye Pohamba wa Namibia

Mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo umeingia siku ya tatu kwa hotuba za viongozi mbali mbali wakigusia masuala ya amani, maendeleo na haki za binadamu wakiangazia ajenda ya maendeleo endelevu baada ya mwaka 2015. Assumpta Massoi amefuatilia na hii ni taarifa yake. (Taarifa ya Assumpta) Kiongozi wa kwanza kutoka Afrika kuhutubia [...]

26/09/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa wataka kutekelezwa kwa haki za binadamu

Kusikiliza / Navi Pillay

Miaka ishirini baada ya mataifa kukubaliana kuhusu njia za kuboresha haki za binadamu, mpangilio wa kimataifa umewekwa na hatua zimepigwa lakini hata hivyo haujatekelzwa kwenye nchi nyingi kwa mujibu wa maafisa kutoka Umoja wa Mataifa. Jason Nyakundi na taarifa kamili: (Taarifa ya Jason) Akiongea kwenye warsha iliyoandaliwa pembeni mwa mkutano mkuu wa Umoja wa Mataia [...]

26/09/2013 | Jamii: Taarifa za dharura | Kusoma Zaidi »

Ukanda wa Sahel bado kuna changamoto, tushirikiane kusaidia: Ban

Kusikiliza / KM Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amezungumza kwenye kikao cha ngazi ya juu kuhusu ukanda wa Sahel na kusema kuwa mwaka mmoja baada ya mjadala kuhusu eneo hilo, juhudi za pamoja zimesaidia kuimarisha hali ya usalama, kisiasa na hata kuna mikakati ya kushughulikia changamoto kubwa. Ripoti ya Alice Kariuki inafafanua zaidi: (Taarifa ya [...]

26/09/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Baraza Kuu laangazia utokomezaji wa silaha za nyuklia, Iran yazungumza

Kusikiliza / Rais Hassan Rouhani wa Iran

Hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, kumefanyika mkutano wa ngazi ya juu kuhusu suala la kutokomeza silaha za nyuklia na kupunguza silaha kwa ujumla. Joshua Mmali amekuwa akiufuatilia mkutano huo. TAARIFA YA JOSHUA Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, John William Ashe, ametoa wito kwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, [...]

26/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Leo ni siku ya kimataifa ya masuala ya shughuli za majini

Kusikiliza / wmd-2013-logo-330

Leo ni siku ya kimataifa ya masuala ya shughulli za majini. Katika ujumbe wake maalumu kuhusu siku hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema siku hii ambayo huadhimishwa Septemba 26 kila mwaka safari hii imeangukia katika wakati muhimu , wakati ambao Umoja wa Mataifa unaongoza katika juhudi za mwisho za kufikia malengo [...]

26/09/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya nchi 100 zaahidi kuchukua hatua dhidi ya ukatili wa kingono na ubakaji vitani:

Kusikiliza / Hawa Bangura

Azimio lililozinduliwa kando ya mjadala wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York lina miakakati ya ya vitendo na kisiasa ya kutokomeza matumizi ya ubakaji na ukatili wa kimapenzi kama silaha ya vita. Nchi 113 zimeidhinisha azimio la kihistoria la kubeba jukumu la kumaliza ukatili wa kimapenzi katika migogoro. Nchi nyingine zinaendelea kuwa [...]

26/09/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Chad yapongezwa kwa juhudi za mchango wa amani Afrika:

Kusikiliza / Rais Idriss Deby wa Chad

Rais wa Chad Idriss Deby Itno amekutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon kandoni mwa mjadala wa baraza kuu la 68. Bam ameipongeza serikali ya Chad kwa juhudi za mchango wake katika kuleta amani barani Afrika na hasa kwa kuchangia vikosi hivi karibuni kwenda kulinda amani nchini Mali. Viongozi hao wawili pia [...]

26/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tanzania yatimiza lengo la kupunguza vifo vya watoto wa chini ya miaka mitano:Mwinyi

Kusikiliza / Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizotimiza lengo la kuzuia vifo vya watoto wa chini ya miaka mitano

Serikali ya Tanzania imesema inajivunia kutanabaisha kwamba lengo la nne la milenia ambalo ni kupunguza vifo vya watoto wa chini ya umri wa miaka mitano limetimizwa tayari ikiwa imesalia miaka miwili kabla ya ukomo wa malengo ya maendeleo ya milenia hapo 2015. Akizungumza na Flora Nducha wa Radio ya Umoja wa Mataifa waziri wa afya [...]

26/09/2013 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031