Nyumbani » 25/09/2013 Entries posted on “Septemba 25th, 2013”

Rais Kagame aongeza sauti yake kwa wakosoaji wa ICC

Kusikiliza / Rais Paul Kagame akilihutubia Baraza Kuu

Rais Paul Kagame wa Rwanda, leo ameongeza zauti yake kwa zile za viongozi wa Afrika ambao wameishutumu mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC, kwa kuwalenga tu viongozi wa Afrika. Katika hotuba yake kwenye mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Jumanne mchana, Bwana Kagame amesema Waafrika waliunga mkono muafaka wa kimataifa wa kuhakikisha [...]

25/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuelekea ukomo MDGS, elimu ya msingi yaboreshwa Tanzania

Kusikiliza / Primary Pupils

Wakati mkutano wa 68 wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa ukiendelea mjini New York huku mjadala mkuu ukiwa ni utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia , Tanzania imepiga hatua katika lengo la pili la elimu kwa wote ambapo takwimu zinasema mwaka jana uwiano wa uandikishaji wa wavulana ulikuwa asilimia 14.4  huku wasichana ikiwa aslimia [...]

25/09/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Ban akutana na mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa yenye wajumbe wa kudumu katika baraza la usalama

Kusikiliza / Bendera za nchi zenye wajumbe wa kudumu katika baraza la usalama

Hii leo mjini New York, kando mwa mikutano ya baraza kuu la Umoja wa Mataifa, Katibu Mkuu Ban Ki-Moon amekuwa na mazungumzo na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi tano wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama ambazo ni China, Urusi, Marekani, Ufaransa na Uingereza. Mazungumzo hayo wakati wa mlo maalum wa mchana yalijikita [...]

25/09/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Rais Kabila ajadili na Ban hali ya Dr Congo

Kusikiliza / Katibu Mkuu, Ban Ki-moon na rais wa DR Congo Joseph Kabila Kabange

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila Kabange leo amekuwa na mkutano na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon kando ya mjadala wa baraza kuu la Umoja wa mataifa. Katika mkutano wao wamebadilishana mawazo kuhusu hali ya Dr Congo na ukanda wote wa maziwa makuu ikiwemo hatua ya mazungumzo ya Kampala. [...]

25/09/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa MONUSCO alaani vikali mashambulizi dhidi ya shule na hospitali:

Kusikiliza / Martin Kobler

  Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (MONUSCO) umelaani vikali mashambulio dhidi ya shule na hospitali yanayofanywa na pande zinazoshirikia vita na hususani kundi la watu wenye silaha la ADF katika eneo la Beni. Mkuu wa MONUSCO Martin Kobler amesema ADF na pandezote zinazoshiriki vitendo hivyo ni lazima waache mara [...]

25/09/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Marekani yasaini mkataba wa udhibiti wa biashara ya silaha, Ban apongeza

Kusikiliza / Katibu Mkuu, Ban Ki-moon

Idadi ya nchi zilizotia saini mkataba wa kimataifa unaodhibiti biashara ya silaha leo imeongezeka na kufikia zaidi ya nusu ya nchi 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa. Kufuatia hatua hiyo Katibu Mkuu wa Ban Ki-moon ambaye ndiye mwangalizi wa mkataba huo hutoa pongezi kwa kila nchi inapotia saini lakini kwa hatua ya leo imekuwa na [...]

25/09/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Hali ya haki za binadamu nchini Sudan yasalia kuwa mbaya:UM

Kusikiliza / Mashood Baderin

Hali ya haki za binadamu nchini  Sudan  inasalia kuwa mbaya huku raia wakinyimwa fursa ya kufurahia haki zao zikiwemo za kisiasa kwa mujibu wa mtaalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa. Mashood A. Baderin ambaye ni mtalaamu anayehusika na hali ya haki za binadamu nchini Sudan amesema kuwa kubana shughuli za mashirika ya [...]

25/09/2013 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ripoti ya UNCTAD kushusu sheria za biasharakwa njia ya mtandao za ASEA yachapishwa

Kusikiliza / Ripoti

Ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la biashara na maendeleo UNCTAD imeelezea hatua kubwa zilizopigwa na nchi za eneo la Kusin mwa Asia ASEAN ambazo zimefanikisha mpango wa biashara kwa njia ya mtandao yaani e-commerce. Ripoti hiyo yenye kichwa cha habari,mapitio ya sheria katika eneo la ASEAN imependekeza kuharakisha mchakato wa muungano wa kikanda [...]

25/09/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tanzania yapiga hatua kutimiza lengo la elimu.

Kusikiliza / wanafunzi shuleni

Wakati mkutano wa 68 wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa ukiendelea mjini New York huku mada kuu ikiwa ni utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia , Tanzania imepiga hatua katika lengo la pili la elimu kwa wote ambapo takwimu zinasema mwaka jana uwiano wa uandikishaji wa wavulana ulikuwa asilimia 14.4  huku wasichana ikiwa [...]

25/09/2013 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Rais Museveni azungumzia ICC na shambulizi la Nairobi

Kusikiliza / Rais Museveni, mkewe Janet na Alice Kariuki wa Redio UM

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesema mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC, imefanya kosa kubwa kwa kupuuza maoni ya viongozi wa Afrika katika azimio walilopitisha kuhusu kesi inayomhusu rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na makamu wake, Willian Ruto, akiongeza kuwa bara la Afrika ni la watu wa Afrika. Katika mahojiano na Redio ya Umoja wa [...]

25/09/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Uhusiano baina ya Sudan na Sudan Kusini wajadiliwa:

Kusikiliza / Ali Ahmed Karti

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na waziri wa mambo ya nje wa Sudan Ali Ahmed Kartiwamekutana na kujadili masuala mbalimbali ikiwemo uhusiano baina ya Sudan na Sudan Kusini, hali ya Darfur, Abyei, Kordofan Kusini na jimbo la Blue Nile Ban amekaribisha matokeo ya mikutano mitatu ya mwezi septemba baina ya Rais [...]

25/09/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Malawi iko mbioni kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia:Banda

Kusikiliza / Rais Joyce Banda wa Malawi

Rais wa Malawi Bi Joyce Banda ameliambia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuwa nchi yake imepata mafanikio makubwa kwenye nyanja mbali mbali tangu achukue madaraka mwaka 2012. Alice Kariuki na taarifa kamili: (RIPOTI YA ALICE KARIUKI) Katika ujumbe wake Bi Banda amesema kuwa kutokana na utekelezaji wa mipango mipya ya kushughulikia changamoto za kisiasa [...]

25/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tutawashinda magaidi wa Al shabaab: Rais Museveni

Kusikiliza / Rais Yoweri Museveni

Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amesema watu waliohusika katika shambulizi la Nairobi na kuwaua raia wasio na hatia watasakwa na kuwajibishwa. Rais Museveni amesema hayo katika mahojiano maalumu na Radio ya Umoja wa Mataifa. Mnamo mwaka 2010, Uganda iliathirika kwa mauaji ya mashambulizi ya mabomu, ambayo yalipangwa na kutekelezwa na kundi la kigaidi la Al [...]

25/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mjumbe wa UM ataka kufanyika kwa mashauriano ya kisiasa nchini Cambodia

Kusikiliza / Ramana ya Cambodia

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya haki za binadamu nchini Cambodia Surya Prasad Subedi amesema kuwa kuwa taifa hilobado lina changamoto nyingi katika kuimarisha na kulinda haki za binadamu. Mjumbe huyo amesema kuwa hata kama uchaguzi wa hivi majuzi ulikuwa wa amani  serikali ilishindwa kuchunguza madai ya udanganyifu wakati wa shughuli [...]

25/09/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Uongozi bora na fedha kusaidia kutimiza lengo la elimu kwa wote:

Kusikiliza / Mtoto shuleni

Wakati duniani kote kuna watoto milioni 57 ambao hahudhurii shule ,suala la uongozi bora na ufadhili wa fedha ni muhimu saana ili kuwapa watoto wengi zaidi fursa ya elimu bora . Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon alizindua mradi maalumu wa kimataifa wa elimu mwaka 2012 ili moja kumuingiza shule kila mtoto, pili [...]

25/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Malengo ya milenia yameleta ahueni kwa watoto, lakini wengi bado wanakumbwa na mkwamo: Ban

Kusikiliza / Malengo ya Milenia,2015

Matukio mbali mbali maalum yamekuwa yakiendelea sambamba na mjadala wa mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa mataifa na miongoni mwa matukio hayo hii leo ni kufanikisha malengo ya maendeleo ya milenia yanayofikia ukomo wake mwakani.  Flora Nducha na taarifa kamili  (RIPOTI YA FLORA NDUCHA) Tukio hilo liliandaliwa na Baraza Kuu ambapo Karibu Mkuu Ban [...]

25/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Viongozi Afrika wakerwa na ICC kumulika viongozi wa Afrika pekee

Kusikiliza / ICC-building3

Suala la mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ICC kuwagusa  viongozi wa Afrika pekee limeibuka wakati wa mkutano baina ya wawakilishi wa nchi za Afrika Mashariki na shirika la kimataifa la maendeleo IGAD ambapo mjadala wa kina kuhusu swala hilo utafanyika Ijumaa wiki hii. Grace Kaneiya anaarifu (RIPOTI YA GRACE KANEIYA) Waziri wa mambo [...]

25/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Soko, umaskini na tamaa vichocheo vya ujangili wa ndovu Tanzania

Kusikiliza / Meno ya ndovu yakiteketezwa

Tanzania imesema ongezeko la bei ya pembe za ndovu huko Mashariki ya Mbali, umaskini wa wananchi na tamaa ya baadhi ya watu ni baadhi ya vichocheo vikubwa kwa ujangili wa tembo nchini humo. Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki amesema hayo katika mahojiano maalum na Idhaa hii mjini New York, Marekani ambako yuko [...]

25/09/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Suala la DR Congo na Misri bado ni changamoto kwa jumuiya ya Kimataifa:

Kusikiliza / Waasi wa M23

  Suala la vikundi vya waasi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo likiwemo kundi la M23 na wanamgambo wengine kama Mayi-Mayi na FDLR badi ni changamoto kwa jumuiya ya kimataifa kama lilivyo suala la kupata suluhu ya kisiasa nchini Misri baada ya kupinduliwa Rais Mohammed Morsi. Hayo yamejiri katika mkutano wa ngazi ya juu wa [...]

25/09/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031