Nyumbani » 24/09/2013 Entries posted on “Septemba 24th, 2013”

Tunaweza kushughulikia tofauti zetu na Marekani: Rais Rouhani

Kusikiliza / Rais wa Iran, Hassan Rouhani

Suala la uhusiano waIran na Marekani pamoja na mpango wa nyuklia wa nchi hiyo ni miongoni mwa mambo yaliyokuwemo kwenye hotuba ya Rais Hassan Rouhani wa Iran alipohutubia kwa mara ya kwanza mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, tangu achaguliwe kushika wadhifa huo hivi karibuni. Rais Rouhani amesema fikra [...]

24/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanachama wa UM waridhia azimio la kukabiliana na ubakaji katika vita

Kusikiliza / Hawa Bangura

Ubakaji katika vita hautakubalika kuendelea tena. Hayo yamesemwa na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili wa kingono katika maeneo ya vita, Bi Zainab Hawa Bangura, kufuatia kupitishwa kwa azimio la kupinga uhalifu huo wa kivita kwenye hafla maalum kando ya mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Bi Bangura amesema kupitishwa [...]

24/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Machafuko ya kidini Nigeria yahitaji suluhu

Kusikiliza / Rais wa Nigeria Goodluck Ebele Jonathan

Machafuko ya kidini ya hivi karibuni nchini Nigeria na hususani katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo ni moja ya ajenda kuu zilizotawala mkutano baina ya Rais Goodluck Ebele Jonathan na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon. Walipokutana kando ya mjadala wa baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wawili hao pia amezungumzia suala [...]

24/09/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Viongozi wa dunia wataka ushirikiano katika mapambano dhidi ya malaria

Kusikiliza / chandarua chenye dawa

Viongozi wa dunia wamekusanyika pamoja kandoni mwa mkutano wa 68 wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa kuzindua mbinu mpya ya kupambana na malaria ugonjwa ambao licha ya juhudi za kuutokomeza bado unaua takribani watu laki sita kila mwaka na hivyo kuwa changamoto kubwa ya maendeleo. Mashirika makuu ya kupambana na maleria lile la kurudisha [...]

24/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban atiwa hofu na hali nchini Maldives:

Kusikiliza / Katibu Mkuu, Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amesema anatiwa hofu na uamuzi wa mahakama kuu nchini Maldives wa kutoa amri ya kuahirisha duru ya pili ya uchaguzi wa Rais uliopangwa kufanyika Septemba 28. Amekumbusha kwamba duru ya kwanza ya uchaguzi hapo Septemba 7 imetambulika kimataifa na kwa waangalizi wa kitaifa kama ulikuwa wa mafanikio. [...]

24/09/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ndoto za walemavu zitatimia iwapo kutakuwepo na dunia jumuishi: Wanyoike- Kibunja

Kusikiliza / Wakati wa mahojiano Assumpta Massoi wa UM Radio, Henry Wanyoike na msaidizi wake Joseph Kibunja

Zaidi ya watu Bilioni Moja duniani wanaishi na ulemavu, na Umoja wa Mataifa unasema kuwa kila uchwao vita na mizozo vinaongeza hatari ya idadi ya walemavu kuongezeka.  Hivyo basi, bila jamii jumuishi, maendeleo endelevu yatakuwa ni ndoto na hata ndoto za walemavu kuweza kuwa na maisha bora yenye hadhi haitaweza kufikiwa. Katika kuhakikisha jamii hiyo [...]

24/09/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Harakati za maendeleo zikiengua baadhi ya maeneo, hazitakuwa endelevu: Zuma

Kusikiliza / Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini akihutubia Baraza Kuu

Harakati mpya za maendeleo duniani zaonekana kutenga na kudidimiza zaidi maeneo maskini duniani, hiyo ni kauli ya Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini akihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York. Ametaja mashauriano ya biashara, udhibiti wa mazingira kwa ajili ya kuinua uchumi kuwa baadhi ya viashirio vya kupuuzwa kwa maendeleo endelevu kwa [...]

24/09/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wakenya watoa maoni yao kuhusu mkutano wa baraza la UM

Kusikiliza / GA Hall

Wakati mkutano wa 68 wa baza kuu la Umoja wa Mataifa ukishika kasi mjiniNew Yorkwananchi wa Kenyawametoa maoniyaokuhusu nini wangependa kijadiliwe katika mkutano huo.   Utatuzi wa migogoro, ajira na mengineyo ni miongoni mwa maoniyao. Ungana na Joseph Msami

24/09/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban akutana na Rais wa Brazili Bi Dilma Rousseff:

Kusikiliza / KM Ban Ki-moon na Rais wa Brazil Dilma Rousseff

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo amekutana na Rais wa Jamhuri ya Brazil Bi Dilma Rousseff. Ban amemshukuru Rais kwa mchango mkubwa wa Brazili katika kuunga mkono masuala ya viupaumbele vya Umoja wa Mataifa. Ban amesema mchango mkubwa wa Brazili kufuatia mkutano wa Rio+20 wa maendeleo endelevu ni suala ambalo halitosahaulika, mchango [...]

24/09/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Shambulio la kigaidi Westgate Kenya ni changamoto ya Kimataifa:

Kusikiliza / Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Bernard Membe

Shambulio la kigaidi lililofanyika mwishoni mwa wiki nchini Kenya limepewa uzito wa juu kwenye mkutano wa viongozi wanaojadili malengo ya maendeleo ya milenia kwenye Baraza Kuu la Umoja wa mataifa. Flora Nducha na taarifa kamili. (TAARIFA YA FLORA NDUCHA) Kwa pamoja viongozi hao wamelaani vikali unyama uliokatili maisha zaidi ya 60 na kujeruhi wengine zaidi [...]

24/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mjadala wa Baraza Kuu wafunguliwa rasmi

Kusikiliza / Ufunguzi rasmi wa kikao cha 68 cha Baraza Kuu

Hatimaye mjadala Mkuu wa kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa umeanza Jumanne mjini New York, Marekani ukijumuisha viongozi wa nchi na mawaziri kutoka nchi 193 wanachama wa Umoja wa huo. Wa Kwanza kuongea amekuwa Katibu Mkuu Ban Ki-Moon na Rais wa Baraza Kuu, John William Ashe. Joshua Mmali ana taarifa kamili: [...]

24/09/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kasi ya kushughulikia changamoto za dunia bado yasuasua: Obama

Kusikiliza / Rais Barack Obama

Rais wa Marekani Barack Obama alikuwa wa pili kuhutubia Baraza Kuu baada ya Rais wa Brazili Bi Dilma Rousseff. Katika hotuba yake Obama amesema kila mwaka nchi wanachama hukutana kujadili mustakhabali wa dunia zikijikita katika amani na usalama na akisema waliounda umoja wa mataifa hawakuwa wajinga bali walifahamu kuwa unahitajika kwa maslahi ya binadamu katika [...]

24/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mjumbe wa UM nchini Somalia anasema kuwa usalama ndiyo changamoto kubwa zaidi nchini Somalia

Kusikiliza / Nicholas Kay

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Nicholas Kay ametoa wito wa kutaka kutolewa kwa msaada ya kifedha na ya kijeshi kusaidia jitihada za muungano wa Afrika katika keleta amani na usalama nchiniSomalia. Taarifa ya Jason Nyakundi ina mengi zaidi (TAARIFA YA JASON NYAKUNDI) Akizungumza mjiniGenevabwana Kay amesema kuwa usalama kwa sasa ndiyo changamoto [...]

24/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Meli yenye chakula cha msaada kwa Wasyria yawasili Beirut

Kusikiliza / Syria wfp

Meli iliyosheheni ngano kutoka Marekani yenye uwezo wa kuwalisha watu milioni 3.5 nchini Syria kwa kipindi cha mwezi mmoja imewasili mjini Beirut nchini lebanon ikiwa ni sehemu ya oparesheni ya dharura ya shirika lampango wa chukula duniani WFP. Alice Kariuki na taarifa kamili: (TAARIFA YA ALICE) Meli hiyo inayofahamika kama MV Mathawee Nareee ilianza safari [...]

24/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ofisi ya haki za binadamu yaitaka Israel ikome ubomoaji wa makazi ya Wapalestina

Kusikiliza /

Serikali ya Israel imelaumiwa kutokana na kitendo chake cha uendeshaji bomoa bomoa kwa makazi ya Wapalestina yaliyoko katika eneo la Ukingo wa Gaza. Inakadiriwa kwamba katika kipindi cha Septemba 16, zaidi ya majengo 58 yalikuwa yamebomolewa ikiwemo yale yaliyokusudiwa kwa ajili ya makazi ya raia. Mamia ya familia ikiwemo watoto wadogo wanataabika kutokana na kukosa [...]

24/09/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ofisi ya Haki za binadamu yakaribisha sheria mpya ya haki nchini Libya

Kusikiliza / Human Rights

Ofisi ya haki za binadamu imekaribisha sheria mpya iliyopitishwa nchini Libya ambayo ambayo inakarinisha kipindi cha mpito kwa taifa hilo. Sheria hiyo inatoa nafasi kuanzishwa tume ya maridhiano itayokuwa na kazi ya kukusanya taarifa zitazisaidia kulivusha taifa hilo linaloandamwa na hali ya mkwamo. Kupitishwa kwa sheria hiyo sasa kunafungua njia ya kuwepo uwanja wa kuheshimiwa [...]

24/09/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Hebu tubadili jinsi tunavyoongoza kwa maslahi ya dunia yetu: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon akihutubia Baraza Kuu

Mjadala Mkuu wa kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa umeanza Jumanne mjini New York, Marekani ukijumuisha viongozi wa nchi na mawaziri kutoka nchi 193 wanachama wa Umoja wa huo. Kabla ya kuanza rasmi kwa mjadala huo Katibu Mkuu Ban Ki-Moon alitumia fursa hiyo kuelezea kazi za ofisi hiyo kuanzia masuala amani [...]

24/09/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UNHCR yalaani ongezeko la mashambulizi Iraq

Kusikiliza / UNHCR/H.Caux

Huko nchini Iraq Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR limesema kuwa linatilia shaka kutonana na ongezeko la mapigano ya wenyewe kwa wenyewe ambayo yamesababisha idadi kubwa ya watu kukosa makazi. Kumekuwa na mfululizo wa matukio ya mashambulizi ya mabomu na maguruneti hali ambayo imezusha hali ya wasiwasi mkubwa kwa wananchi. George Njogopa [...]

24/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya kibinadamu ya zaidi ya watu 150,000 Ufilipino inatia hofu: OCHA

Kusikiliza / Philippines OCHA

Ofisi ya kuratibu misaada ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, OCHA imeelezea wasiwasi wake kuhusu hali ya kibinadamu ya takriban watu 158,000 ambao wameathiriwa na mapigano kati ya kundi la wanamgambo wa Moro National Liberation Front na wanajeshi wa serikali katika mji wa Zamboanga na Mkoa wa Basilan Kusini mwa Ufilipino. Tangu Septemba 9, watu [...]

24/09/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kila binadamu anastahili kuvuta hewa safi, biashara ya hewa ya ukaa bado changamoto: Tanzania

Kusikiliza / Dr. Trezya Luoga-Huviza

Lengo namba saba la maendeleo ya Milenia linahusika na uhifadhi wa mazingira ili dunia iweze kuwa mustakhbali endelevu lakini bado inaelezwa kuwa uzalishaji wa hewa chafuzi unaendelea kutishia siyo tu uhai wa binadamu bali pia dunia yenyewe na binadamu hatokuwa na pakukimbilia. Na hivyo katika mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaoanza [...]

24/09/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Waloshambulia kambi ya Asharaf Iraq ni lazima wawajibishwe kisheria:UM

Kusikiliza / Ofisi ya Haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa

  Ofisi ya haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa imeiomba tena serikali ya Iraq kufanya kila iwezalo ili kuwatambua na kuwawajibisha kisheria waliotekeleza shambulizi dhidi ya kambi ya Ashraf, ambako watu 52 waliuawa. Mnamo Septemba 3, ofisi hiyo ilitoa taarifa ya kulaani shambulizi hilo, na kutoa wito kwa serikali ya Iraq kufanya uchunguzi ili [...]

24/09/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Malawi yapiga hatua katika kuwajumuisha walemavu kwenye ajenda ya maendeleo

Kusikiliza / Ulemavu, malawi

Tatizo la ulemavu ni kubwa , ikikadiriwa kuwa watu takribani   watu bilioni moja wanaishi na aina Fulani ya ulemavu. Kila nchi   inachagizwa na Umoja wa Mataifa kuhakikisha mipangoyaoya baada ya mwaka 2015 inajumuisha mahitaji na mchango wa walemavu katika kuleta maendeleo endelevu, kwani bila kuwakwamua walemavu maendeleo endelevu itakuwa ni ndoto. Mataifa mbalimbali sasa yameanza [...]

24/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kenya imechukua hatua kujumuisha walemavu: Wanyoike

Kusikiliza / mwanariadha Henry wanyoike na msaidizi wakeJoseph Kibunja

Wakati mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ukianza leo New York, Marekani ajenda muhimu ikiwa ni utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia na ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015, mwanariadha mashuhuri kutoka Kenya mwenye ulemavu wa macho Henry Wanyoike amesema hatua zimepigwa kusaidia kundi hilo lakini bado kuna changamoto. Akizungumza [...]

24/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031