Nyumbani » 23/09/2013 Entries posted on “Septemba 23rd, 2013”

Dola bilioni 2.5 zachangishwa katika ahadi mpya za kufikia malengo ya kukabiliana na umaskini duniani

Kusikiliza / MDGs

Ahadi za ziada za kupiga jeki ufikiaji wa malengo ya maendeleo ya milenia zimetangazwa leo, na hivyo kufikisha dola bilioni 2.5 katika ahadi mpya, kabla ya tarehe ya ukomo wa malengo ya maendeleo ya milenia. Waziri wa Uingereza wa Maendeleo ya Kimataifa, Justine Greening, ametangaza mchango mpya wa serikali ya Uingereza kwa mfuko wa kimataifa [...]

23/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tovuti ya kimataifa ya ufahamu yazinduliwa kuimarisha nguvu za wanawake kiuchumi

Kusikiliza / unwomen_logo_500

Wakati wa kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kitengo cha maswala ya wanawake katika Umoja wa Mataifa, UN Women, kwa ushirikiano na serikali ya Canada, leo wamezindua uwanja wa kimataifa wa kuwapa wanawake ufahamu wa kujiimarisha kiuchumi, ambao utakuwa ni tovuti ya (www.empowerwomen.org). Uwanja huu wa mafunzo ulo wazi kwenye tovuti, [...]

23/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban akutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Côte d'Ivoire

Kusikiliza / Alassane Ouattara

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kin-moon leo amekutana na kufanya mazungumzo na rais wa Côte d'Ivoire Alassane Ouattara. Viongozi hao wamejadili mafanikio yaliyofikiwa na Côte d'Ivoire tangu kuzuka kwa mgogoro kabla ya uchaguzi nchini humo na muundo wa Umoja wa Mataifa katika ujumbe wa umoja huo nchini Côte d'Ivoire UNOCI pamoja na hali [...]

23/09/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Watoto badio wanateseka kufuatia mgogoro Syria:UNICEF

Kusikiliza / Watoto Syria

  Wakati mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaanza kesho mjini New York shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linaonya kwamba ni lazima watoto wanoteseka kufuatia vita vinavyoendelea nchini Syria wakombolewe. Mkurugenzi Mkuu wa UNICEF Anthony Lake amesema kuendelea kwa vita nchini humo kunamaanisha kuendelea kutopata huduma kwa watoto kama [...]

23/09/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Viongozi wakutana kuhusu amani DRC na ukanda wa Maziwa Makuu

Kusikiliza / Ban na Dlamini-Zuma

Kuna uwezekano wa kupata amani, usalama na ushirikiano katika eneo la Maziwa Makuu, licha ya changamoto nyingi za kiusalama na kibinadamu. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Ban Ki-Moon, wakati wa mkutano wa ngazi ya juu kuhusu amani, usalama na ushirikiano  kwa ajili ya eneo la Maziwa Makuu, ambao umefanyika leo kwenye makao makuu ya Umoja [...]

23/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tanzania yapiga hatua kudhibiti vifo vya wajawazito

Kusikiliza / Mwanamke mjamzito

Utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia, MDGS ni moja ya agenda muhimu wakati mkutano wa 68 wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa uanotarajiwa kuanza mnamo September 23 mwaka huu mjiniNew York. Ungana na Tamimu Adam kutoka radio washirika , Jogoo Fm mkoani Ruvuma katika makala inayoangazia namna utekelezaji wa lengo la tano la [...]

23/09/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

ILO yatoa takwimu kuhusiana na kupungua kwa ajira za watoto

Kusikiliza / Ajira ya watoto

Ripoti mpya iliyotolewa na shirika la kazi duniani ILO, imesema kuwa kiwango cha ajira ya watoto duniani kimepungua kwa wastani wa theluthi moj hatua ambayo inaashiria mafanikio katika siku za usoni Kiwango hicho ambacho ni cha mara ya kwanza tangu mwaka 2000 kimepungua kutoka watoto milioni 246 hadi kufikia milioni 168. Hata hivyo ripoti hiyo [...]

23/09/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

ICC yamruhusu Ruto arejee Nairobi kufuatia sakata linaloendelea Westgate

Kusikiliza / Naibu rais wa Kenya, William Ruto

Majaji wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wanaosikiliza kesi dhidi ya Makamu wa rais wa Kenya William Ruto, wamemruhusu mshtakiwa huyo kurejea nyumbani kwa wiki moja ili kuweza kushughulikia sakata linaloendelelea kwenye eneo la manunuzi la Westgate mjini Nairobi Kenya. Uamuzi huo ulitangazwa haraka mahakamani leo na Jaji Chile Eboe-Osuji ambapo mara moja Ruto alielekezwa [...]

23/09/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban akutana na Marais wa Malawi na Namibia:

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban akutana na rais Hilde wa Malawi na rais Hifikepunye wa Namibia

Rais wa Malawi Bi Joyce Hilda Mtila Banda ambaye pia ndiye mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya maendeleo kwa nchi za Kusini mwa Afrika SADC pamoja na Rais wa Namibia Bwana Hifikepunye Pohamba wamekutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon hapa New York kando ya mjadala wa baraza kuu. Katika mkutano wao [...]

23/09/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya watu 60 wauawa kwenye shambulizi la kigaidi nchini Kenya

Kusikiliza / Harakati za Red Cross katika eneo la shambulizi, West gate, Nairobi

Takriban watu 62 wameripotiwa kuuawa na wengine zaidi ya 150 wakijeruhiwa baada ya watu waliojihami wanaokisiwa kuwa wanamgambo wa kundi la Al shabaab kushambulia jumba moja lenye maduka mengi kwenye mji mkuu waKenyaNairobi. Zaidi ya watu 1000 waliokolewa kutoka kwenye jumba hilo la Westgate ambapo pia hadi sasa watu kadha wanakisiwa kushikiliwa na magaidi hao. [...]

23/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban ataka vitendo ili kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia

Kusikiliza / MDGs

Katibu Mkuu wa Umoja wa Matifa Ban Ki-moon amezungumza wakati wa uzinduzi wa mkutano wa kuchagiza kuimarisha ushirikiano katika kufanikisha kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia na kusema ni muhimu kutekeleza kwa vitendo na sio nadharia pekee ili kutimiza malengo hayo. Taarifa zaidi na Joseph Msami. (TAARIFA YA MSAMI) Katibu huyo mkuu wa Umoja wa [...]

23/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI miongoni mwa vijana yapungua kwa kiwango kikubwa:UN

Kusikiliza / UNAIDS youth

Shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na Ukimwi,UNAIDS limesema kuwa maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi miongoni mwa vijana yamepungua kwa kiwango cha kuridhisha kwa  asilimia 52 huku watu wazima yakipungua kwa asilimia 33. Kupungua huko kumerekodiwa kuanzia mwaka 2001 Takwimu hizo zimetolewa katika wakati ambapo viongozi wa kimataifa wakijaandaa kukutana mjini New York [...]

23/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uganda yawa chonjo kuimarisha ulinzi

Kusikiliza / Nchi Uganda ambayo inapkana na Kenya

Tukio la Kenya limezua hofu katika nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Uganda kama anavyoripoti John Kibego wa radio washirika ya Spice FM kutokaUganda. (Taarifa ya John Kibego) Hofu imetanda kuwa huenda walioshanbulia jengo la WSestgate mjini Niarobi wakageukiaUganda. Vicent Senyunja raia wa kawaida anaeleza kwa nini anaogopa. Mkaguzi Mku wa Polisi Gen. Kale Kayihura amesema [...]

23/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ushirikiano baina ya UM na Muungano wa Afrika muhimu: Ban /Nkosazana Dlamini Zuma

Kusikiliza / Katibu MKuu Ban Ki-moon na mwenyekiti wa AU Nkosazana Dlamini-Zuma

Mwenyekiti wa Tume ya Muungano wa Afrika na Bi Nkosazana Dlamini-Zuma, na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon wakutana kando ya kikao cha baraza Kuu la Umoja wa mataifa. Viongozi hao wawili wamebadilishana mawazo kuhusu juhudi za kuboresha ushirikiano na operesheni za pamoja za Umoja wa mataifa na Muungano wa Afrika. Ban amemshukuru [...]

23/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban amelaani vikali shambulio la kanisani nchini Pakistan:

Kusikiliza / Ramana ya Pakistan

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa amelaani vikali shambulio la kigaidi la Jumapili ndani ya kanisa la Kikristo huko Peshawar, Pakistan, ambalo limearifiwa kukatili maisha ya watu zaidi ya 75 na kujeruhi wengine zaidi ya 100 ambao ni wamuni waliokuwa wakihudhuria misa. Ban Ki-moon amesema shambulio hilo la bomu la kujitoa muhanga ni kitendo cha [...]

23/09/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Fursa sawa kwa makundi yote kuelekea ajenda ya maendeleo baada ya 2015

Kusikiliza / Dkt.John Ashe, Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa

katika kuelekea kuanza kwa mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hapo kesho Jumanne, hii leo baraza hilo limekuwa na kikao cha ngazi ya juu kuhusu kufikia malengo ya maendeleo ya milenia na malengo mengine ya kimataifa kuhusu watu wenye ulemavu. Joshua Mmali Massoi na taarifa zaidi. (Taarifa ya Joshua) Kikao hicho cha ngazi [...]

23/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Suala la Syria na Libya la tawala mkutano wa Ban na Dr. Nabil Elaraby

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amekutana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya nchi za Kiarabu Dr. Nabil Elaraby. Mazungumzo yao yametawaliwa na hali inayoendelea nchini Syria, Libya na hali nzima ya mchakato wa amani Mashariki ya Kati. Kwa pamoja wamesisitiza haja ya kukomesha umwagaji damu nchini Syria haraka iwezekanavyo pia kushughulikia haraka [...]

23/09/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban azungumza na waziri Wang Yi, wa China

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon na waziri Wang Yi

Katibu Mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon ameishukuru serikali ya Uchina kwa jukumu kubwa na mchango wake wa uongozi kwenye masuala ya Umoja wa Mataifa. Akizungumza na waziri wa mambo ya nje wan chi hiyo Wang Yi, ameishukuru serikali hiyo hususani kwa msaada wa mpango wa ulinzi wa Umoja wa mataifa na mchango wake [...]

23/09/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Tanzania yapunguza vifo vya wajawazito kwa asilimia 21

Kusikiliza / Mjamzito akipatiwa huduma katika moja ya kliniki nchini Tanzania

Katika kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia hususani lengo la tano la kupunguza vifo vya wajawazito, serikali yaTanzaniakupitia wizara ya afya inasema imepunguza vifo hivyo hivyo. Takwimu za wizara ya afya zinaonyesha kuwa vifo vya wajawazito vimepungua kwa asilimia 21 kutoka vifo 578  kwa kila uzazi hai Laki Moja kati ya mwaka 2004-2005 hadi vifo [...]

23/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031