Nyumbani » 20/09/2013 Entries posted on “Septemba 20th, 2013”

Ban akutana na kuzungumza na Waziri Mkuu wa Uganda

Kusikiliza / Mheshimiwa Amama Mbabazi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Uganda Amama Mbabazi ambapo viongozi hao wamezungumzia utekelezaji wa mkataba wa amani, usalama na ushirikiano kwa ajili ya Jamhuri ya Kidemokarsia ya kongo, DRC na ukanda wa maziwa makuu. Katika mazungumzo hayo Bwana Ban ameelezea kuridhishwa kwake na [...]

20/09/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Migomo ya elimu iepukwe kunusuru mustakabali wa elimu:UNESCO

Kusikiliza / wanafunzi shuleni

  Migomo katika sekta ya elimu hudidimiza kiwango cha elimu katika eneo husika na hivyo kuzorotesha maendeleo, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO. Katika kuangazia hili afisa wa UNESCO nchini Tanzania Elizabeth Kyondo anasema ni muhimu mazingira ya walimu yakaboreshwa ili wafanye kazi zao kwa ufanisi ili kuleta tija katika [...]

20/09/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Vimbunga vyasababisha maafa Mexico: Ban atuma rambirambi

Kusikiliza / Mwananchi wa Mexico akijitahidi kukabiliana na mafuriko yatokanayo na kimbunga Manuel

Wakati maafa yaliyotokana na vimbunga Manuel na Ingrid yakiendelea kuwa dhahiri, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameeleza kushtushwa kwake na vifo vya watu kutokana na janga hilo pamoja na uharibifu wa mali na makazi. Vimbunga hivyo vilivyoanza tarehe 17 mwezi huu vimeathiri watu zaidi ya Milioni Moja huku hali ya tahadhari ikiwa [...]

20/09/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mshoromoni Mombasa, Kenya na harakati za kupambana na Ukimwi

Kusikiliza / Dawa

Ripoti mpya ya mfuko wa kimataifa wa kupambana na Ukimwi, Malaria na Kifua Kikuu, Global Fund imesema mafanikio makubwa yamepatikana katika kupambana na magonjwa hayo. Kubwa zaidi ni utoaji wa dawa za kupunguza makali ya virusi hivyo kwa makundi mbali mbali mbali ikiwemo wajawazito, elimu ya kinga na kadhalika. Mafaniko hayo yametangazwa wakati huu ambapo [...]

20/09/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Sikuagiza sanamu ya Waziri Mkuu ing'olewe" Pillay

Kusikiliza / Bi. Navi Pillay wakati wa ziara yake nchi Sri Lanka hivi karibuni

Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema Kamishna mkuu Navi Pillay kamwe hakutoa maoni yoyote kuhusu sanamu ya Waziri Mkuu DS Senanayake na kwamba hakuna mahali popote wakati wa ziara yake nchini humo ambapo aliagiza sanamu hiyo iondolewe. Kauli  ya ofisi hiyo imetolewa baada ya kusambaa kwa taarifa hizo potofu ambapo tayari [...]

20/09/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mtu mmoja kati ya saba anaishi na aina Fulani ya ulemavu: WHO

Kusikiliza / Nembo ya WHO

Kwa upande wa afya imebainika kuwa mtu mmoja kati ya saba duniani anaishi na aina Fulani ya ulemavu limesema shirika la afya duniani WHO. Kwa mujibu wa shirika hilo wengi wa watu hao wanakabiliwa na vikwazo katika kupata huduma za afya na hivyo kuwaacha katika hali ya kutopata huduma zinazotakiwa , matokeo mabaya ya kiafya [...]

20/09/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

WFP yahofia hali watu walonaswa katikati ya mapigano Syria

Kusikiliza / WFP Syria

  Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema kuwa limeingiwa na wasiwasi kufuatia idadi kubwa ya watu kunaswa katika miji ya Syria ikiwemo Damascus katika wakati ambapo mapigano yakiendelea kuchacha. WFP imeanzisha juhudi za kusambaza misaada ya chakula kwa watu zaidi ya milioni 3 katika kipindi cha mwezi huu na tayari imetoa mwito kwa [...]

20/09/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Bila uongozi wa kisheria hakuna usalama wala uwajibikaji: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu

Bila uongozi wa kisheria, hakuwezi kuwa na usalama au uwajibikaji, na ukiukwaji wa haki za binadamu hutendeka bila kukabiliwa kisheria. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon wakati akipokea tuzo ya Uongozi wa Kisheria ya LexisNexis jana jioni kwa niaba ya UM. Tuzo hiyo imetolewa na mashirika mawili: lile la LexisNexis ambalo linajishulisha [...]

20/09/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

IRAN wekeni fursa bayana kwa watetezi wa haki za binadamu: Pillay

Kusikiliza / Navi Pillay

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesifu hatua yaIranya kuachia huru mapema wiki hi wafungwa 12 wa kisiasa nchini humo huku akiisihi serikali kuchukua hatua murua za kumaliza unyanyasaji dhidi ya watetezi wa haki za binadamu. Taarifa zaidi na Jason Nyakundi: (Taarifa ya Jason) Kati ya wale walioachiliwa ni [...]

20/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mnahitajika kuandaa mustakhbali wa dunia hii, Ban awaeleza washiriki wa kikao cha viongozi

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amezungumza kwenye kikao cha viongozi kijulikanacho kama Global Compact Leaders na kusema kuwa wao ndio wanaotegemewa katika kuandaa mustakhbali endelevu wa dunia. Ripoti ya Joseph Msami inafafanua zaidi. (Taarifa ya Joseph Msami) Vitendo vyenu vinahesabika na tunawahitaji ninyi muwe waandaji wa mustakhbali endelevu, ni kauli ya Bwana [...]

20/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mafanikio makubwa yapatikana katika kukabiliana na Ukimwi

Kusikiliza / Mkuu wa Global Fund, Mark Dybul

Mfuko wa kimataifa wa kupambana na ukimwi, Malaria na Kifua Kikuu, Global Fund umetangaza hii leo mafanikio makubwa yaliyopatikana katika matibabu kwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi pamoja na kinga kwa maambukizi ya virusi hivyo kutoka kwa mama kwenda kwamtoto. Matokeo yanaonyesha kuwa hadi Julai mwaka huu watu milioni mano nukta tatu wanaoishi na [...]

20/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mzozo nchini CAR watishia usalama wa watoto: UNICEF

Kusikiliza / car children2

Takribani watoto 3,500 wametumikishwa katika vikundi mbali mbali vyenye silaha huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, na hiyo ni kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF. Shirika hilo linasema jeshi la serikali na vikundi vya waasi vimekuwa vikitumikisha jeshini watoto wa kike na wa kiume tangu kuanza kwa mzozo huo [...]

20/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Machafuko mapya yazuka CAR

Kusikiliza / CAR

Ripoti kutoka Jamhuri ya Kati zinasema kuwa, mamia ya watu wamekosa makazi kutokana na mapigano yaliyoibuka upya katika eneo la Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo. Mapigano hayo yameripotiwa kuibuka siku ya jumamosi na jumanne, yakihusisha makundi ya wanamgambo ambao hata hivyo hawakufahamika mara moja.  Hali ya wasiwasi na taharuki uliikumba miji ya Bossembele na Bossangoa [...]

20/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yahitaji dola milioni $21.4 zaidi kwa wakimbizi wa DRC walioko Uganda

Kusikiliza / Wakimbizi wa DRC walioko Uganda

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR, limesema linahitaji kwa dharura zaidi ya dola Milioni 21.4 kwa ajili ya operesheni zake nchini Uganda ambazo zinakabiliwa na uhaba wa ufadhili, ili kuwasaidia wakimbizi kutoka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Grace Kaneiya na ripoti kamili. (Taarifa ya Grace) Kiasi hicho cha fedha kitaweza [...]

20/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031