Nyumbani » 19/09/2013 Entries posted on “Septemba 19th, 2013”

Ban alaani shambulizi Kosovo

Kusikiliza / Ramani ya Kosovo

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amelaani shambulizi dhidi ya ujumbe wa Umoja wa Ulaya wa utawala wa kisheria huko Kosovo (EULEX) lililotokea leo Kaskazini mwa Kosovo na kusababisha kifo cha mjumbe mmoja wa ujumbe huo.   Katika taarifa iloyotolewa mjiniNew Yorkleo Bwana Ban ametaka uchunguzi wa haraka na kina [...]

19/09/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban ataka demokrasia kuchukua mkondo wake Maldives

Kusikiliza / Ramana ya Maldives

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema anafuatilia kwa makini hali nchini Maldives kufuatia awamu ya kwanza ya uchaguzi Septemba 7 mwaka huu. Katika taarifa yake iliyotolewa mjini New York Bwana Ban amesema awamu ya kwanza ya uchaguzi ilitambuliwa na waangalizi kimataifa na kitaifa kwa mafanikio . Katibu Mkuu huyo wa Umoja [...]

19/09/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa UM azungumzia hatua za ushirikiano wa kimataifa kwa maendeleo:

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Kumekuwa na hatua kubwa katika kufikia lengo la ushirikiano wa kimataifa kwa ajili ya maendeleo ambalo ni lengo nambari 8 la milenia kati ya malengo yaliyoafikiwa na viongozi wa dunia mwaka 2000 kutokomeza umasikini. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon wakati wa uzinduzi wa ripoti ya mwaka 2013 ya kitengo [...]

19/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Licha ya mashambulizi bado kuna matumaini ya ujenzi wa taifa Somalia

Kusikiliza / Mogadishu

  Wiki hii kiasi cha Euro bilioni 2.4 zimeahidiwa katika kongamano liitwalo New Deal kuhusuSomalia, linayofanyikaBrussels. Ijapokuwa kumekuwa na changamoto, Hatua zimepigwa chini ya Serikali inayoongozwa na rais Hassan Sheik Mohamud , hususani kukuza uchumi wa taifa hilo ambalo limeshuhudia mapigano kwa takribani miongo miwili. Je ninini mustskabali wa Somalia? Ungana na Joseph Msami katika ripoti [...]

19/09/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Uridhiaji wa kimataifa wa mkataba wa haki za watoto unahitajika ili kuwalinda:

Kusikiliza / Leila zerrougui

Mwakilishi maalumu wa watoto na vita vya silaha Bi Leila Zerrougui na mwakilishi maalumu wa ukatili dhidi ya watoto Marta Santos Pais leo wametoa wito wa kimataifa wa kuridhia mkataba wa haki za mtoto na vipengee vyake vitatu. Wawakilishi hao wamesema mamilioni ya watoto duniani wanakabiliwa na machafuko, kunyonywa na ukatili. Na kwa kuwa wamepuuzwa [...]

19/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Demokrasia imepiga hatua, juhudi zaidi zinahitajikai :UM

Kusikiliza / Ján Kubiš, wakati wa kikao, Baraza la Usalama

Licha ya machafuko ya mara kwa mara, Afghanistan imepiga hatua kijamii na mahusiano ya kimataifa na juhudi zaidi zinahitajika katika  taifa hilo linapoelekea katika uchaguzi mkuu mwakani. Akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililojadili hali nchini humo, mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan Jan [...]

19/09/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

IOM yaendelea kuwasaidia wananchi wa Jonglei Sudan Kusini:

Kusikiliza / IOM, Sudan

Shirika la Kiamataifa la uhamaijai IOM linazidi kupeleka misaada Sudan Kusini katika jimbo la Jonglei kufuatioa migogoro ya wwneyewe kwa wwenyewe iliyoathiri watu wa eneohilokwa muda mrefu. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM .  (SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)

19/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nchi 172 kushiriki kongamano la nne la kukabiliana na utumiaji madawa kwenye michezo

Kusikiliza / Nembo ya UNESCO

Kongamano la nne la vyama kwa ajili ya kukabiliana na vitendo vya matumizi ya dawa za kuongeza mguvu kwenye michezo hufanyika kila baada ya miaka mine, na hii ni kulingana na mwongozo uliowekwa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na elimu, sayansi na utamaduni UNESCO. Kongamano hilo ambalo hufanyika makao makuu ya UNESCO Paris, [...]

19/09/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNCTAD yahimiza uanzishwaji wa kilimo mchanganyiko

Kusikiliza / Mkulima shambani, Kenya

Ripoti iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na biashara na maendeleo UNCATD, imesema nchi maskini pamoja na zile tajiri ambazo hujishughulisha na kilimo cha aina moja zinapaswa kubadilisha mkondo na kuhamia katika kilimo chenye mkusanyiko mwingi wa mazao. UNACTD imesema kuwa, nchi hizo pia zinapaswa kuchukua jukumu la kupunguza matumizi ya pembeb jeo [...]

19/09/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Rwanda yaongoza kuwa wabunge wengi wanawake duniani:IPU

Kusikiliza / Jengo la IPU

Muungano wa mabunge duniani IPU unasema wabunge wanawake nchini Rwanda hivi sasa ni karibu theluthi mbili ya wabunge wote kufuatia uchaguzi uliofanyika wiki hii. IPU inasema kwa mujibu wa tume ya uchaguzi ya Rwanda takribani asilimia 64 ya viti vyote vya bunge la chini vinashikiliwa na wanawake ikiwa ni ongezeko kubwa kutoka asilimia 56.3 ya [...]

19/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu 690 wauawa katika machafuko ya Boko Haram Nigeria tangu Mai:OCHA

Kusikiliza / Baada ya shambulio na Boko Haram, Nigeria mwezi Mai

Machafuko na ukosefu wa utulivu unaendelea Kaskazini Mashariki mwaNigeriakukiwa na mapigano zaidi baina ya kundi la kidini la Boko Haram na vikosi vya serikali na washirika wake. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa Agost na shirika la Umoja wa mataifa la masuala ya kibinadamu na msaada wa dharura OCHA idadi ya imeongezeka kwa watu 153 waliouawa [...]

19/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Fursa za kibiashara, madawa na teknolojia zitasaidia kufikia malengo ya umasikini:UM

Kusikiliza / MDGS

Ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu hatua zilizopigwa kufikia malengo ya maendeleo ya milenia ya kutokomeza umasikini inasema hatua zimepigwa katika nchi zinazoendelea kwa upande wa teknolojia, masoko ya nje, upatikanaji wa madawa na kupunguza mzigo wa madeni lakini jumuiya ya kimataifa inatakiwa kuongeza msaada na kufikia muafaka wa kibiashara. Joseph Msami na maelezo zaidi [...]

19/09/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Baraza Kuu latakiwa kuchukua hatua kuhakikisha amani inapatikana

Kusikiliza / Alfred de Zayas

Mtaalamu huru wa Umoja wa mataifa katika kuchagiza demokrasia na utulivu wa kimataifa Alfred de Zayas Alhamisi amelitaka baraza kuu la Umoja wa mataifa kuchukua jukumu muhimu la kuleta na kulinda amani. Pia ametaka jukumu makini zaidi kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Matauifa katika kutoa onyo na hatua za haraka kusuluhisha mivutano katika baraza [...]

19/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uchaguzi ujao Sri Lanka ni muhimu kwa maridhiano ya kisaiasa:Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, ameukaribisha uchaguzi ujao wa mikoani nchini Sri Lanka mnamo Septemba 21, hususan katika Mkoa wa Kaskazini ambako huu utakuwa uchaguzi wa kwanza tangu mabaraza ya mikoa yalipoundwa mnamo mwaka 1987. Katika taarifa iliotolewa na msemaji wake, Bwana Ban amesema anauona uchaguzi huo kama nafasi muhimu ya kuleta [...]

19/09/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Takwimu mpya za UNESCO zadhihirisha jinsi elimu inavyochangia maendeleo

Kusikiliza / Watoto darasani

Iwapo watoto wote wangalipata elimu, mapato ya kila mtu yangaliongezeka kwa asilimia 23 katika kipindi cha miaka 40. Hayo ni kwa mujibu wa takwimu mpya za Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni katika Umoja wa Mataifa, UNESCO. Takwimu za UNESCO zinaonyesha pia kuwa iwapo wanawake wote wangalipata elimu ya msingi, ndoa za watoto na vifo [...]

19/09/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031