Nyumbani » 18/09/2013 Entries posted on “Septemba 18th, 2013”

ICC yaonya kuhusu ushawishi na kuweka hadharani mashahidi

Kusikiliza / Jengo la ICC

Jaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, ambaye anaisikiliza kesi dhidi ya Makamu wa Rais wa Kenya, William Samoei Ruto na mtangazaji Joshua Arap Sang, ametoa taarifa ya kukumbusha kuhusu umuhimu wa kuwalinda mashahidi na kuonya kuwa vitendo vyovyote ambavyo vitazuia upatikanaji wa haki vitakabiliwa kisheriaa. Akiongea mwanzoni mwa kikao cha mchana cha kusikilizwa [...]

18/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Majaji wa ICC waitaka serikali ya Marekani kumkamata Rais Bashir

Kusikiliza / Rais Al-Bashir

    Kufuatia habari kuwa huenda Rais Omar Al Bashir wa Sudan akasafiri hadi Marekani kwa ajili ya mkutano wa viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, imetoa ombi kwa mamlaka za Marekani kumkamata Bwana Bashir na kumwasilisha kwa mahakama hiyo iwapo ataingia kwenye eneo la nchi hiyo. [...]

18/09/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ofisi za kisiasa za UM zina mchango mkubwa wa amani na usalama duniani:Ban

Kusikiliza / Mwangalizi wa UM kwa iliyokuwa ofisi ya UM huko Nepal, UNMIN ambayo imemaliza muda wake.

Ofisi za kisiasa za Umoja wa Mataifa zinazofanya kazi kwenye mazingira hatari duniani kote zimethibitisha kuleta tofauti kubwa kwa kuondoa mvutano na hata kuwezesha nchi kuepuka kutumbukia katika migogoro mikubwa. Hiyo ni sehemu ya yaliyomo kwenye ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon  iliyotolewa leo kwa Baraza Kuu ikiangazia historia ya ofisi [...]

18/09/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UNESCO yadhibitisha uporaji wa makumbusho ya Mallawi Misri:

Kusikiliza / Makumbusho Misri

    Ujumbe wa wataalamu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO nchini Misri umethibitisha kwamba karibu kila kitu cha makumbusho ya taifa ya Mallawi yaliyoko Minya, Kaskazini mwa Misri yameporwa wakati wa machafuko ya mwezi Agost.   Ujumbe uliotayarishwa na wizara ya mambo ya kale ya Misri na uongozi [...]

18/09/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Watoto wakimbizi wa Syria walioko Iraq wasaidiwa vifaa vya shule

Watoto wakimbizi wa Syria

Wakati sintofahamu ikiendelea kuikumba Syria kufauatia machafuko yanayoendelea kwa takribani mwaka wa tatu sasa, hali ya kielimu kwa watoto ni mabya  wakati huu ambapo taarifa zinasema shule nyingi nchini humo ni makazi ya wakimbizi huku nyingine zikibomolewa.   Lakini kuna habari njema kwa watoto walioko katika kambi ya wakimbizi nchini Iraq ambapo wamepatiwa msaada wa [...]

18/09/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Nchi nne za afrika zaafikiana mpango wa udhibiti wa maji:

Kusikiliza / nubian-640x425

Katika juhudi za kuboresha udhibiti wa vyanzo vya maji, mataifa manne ya ya Kaskazini Mashariki mwa Afrika Jumatano yameafikiana kwenye mkutano wa 57 wa shirika la kimataifa la nguvu za atomiki IAEA mjini Vienna, kuanzisha mkakati wa muda mrefu wa utumiaji na udhibiti wa mifumo ya maji. Flora Nducha na taarifa kamili. (TAARIFA YA FLORA [...]

18/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku ya amani yaadhimishwa Umoja wa Mataifa

Kusikiliza / Katibu Mkuu akipiga kengele ya amani

Hafla maalumu ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Amani imefanyika hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, ambako kengele ya amani hupigwa kama sehemu ya kuwakumbuka waliouawa na manusura wa vita, pamoja na kuchagiza uwekaji chini silaha pale ambako vita vinaendelea. Joshua Mmali amefuatilia tukio hilo muhimu Ni mlio wa kengele ya amani, [...]

18/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Chad yaapa kuangamiza njaa na kuongeza mazao ya kilimo:UNDP

Wakazi wa eneo la Dar Sila, Chad, linalokabiliwa na athari za mabadiliko ya tabianchi

Taifa la Chad litajikita kwenye mpango wa kupambana na tatizo la ukosefu wa chakula kwa kuangazia zaidi malengo ya maendeleo ya milenia, taifa ambalo hadi asilimia 25 ya wenyeji wake huenda wakakabiliwa na njaa huku zaidi ya thuluthi moja ya watoto wakiwa na utapiamlo. Jason nyakundi na taarifa kamili. (RIPOTI YA JASON NYAKUNDI) Mkuu wa [...]

18/09/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mke wa Rais wa Uganda aongeza juhudi za ahadi ya vita dhidi ya ukimwi:

Kusikiliza / Bi Janet Museveni

Mke wa Rais wa Uganda Bi Janet K Museveni, amedhihirisha juhudi zake za kukomesha maambukizi mapya ya virusi vya HIV kwa watoto kwa kupeleka kampeni ya kitaifa katika eneo la Karamoja, moja ya mikoa isiyojiweza katika nchi hiyo. Bi Musevern amezindua kampeni ya "kutokomeza maambukizi ya HIV toka kwa mama kwenda kwa motto" Septemba 16 [...]

18/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa ILO waangazia faida za kuajiri watu wenye ulemavu

Kusikiliza / kigali disabled

Wawakilishi kutoka shirika la kazi duniani, ILO na kampuni za kimataifa zaidi ya 20 wanakutana huko Shanghai, China kujadili na kubadilishana uzoefu juu ya manufaa ya kuajiri watu wenye ulemavu. George Njogopa na taarifa kamili. (Taarifa ya George) Wakati wa mkutano huo washiriki walidhihirisha kuwa watu wenye ulemavu wanaweza kujumuishwa kwa mafanikio makubwa kwenye nguvu [...]

18/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nishati ya atomiki na uangamizi wa wadudu waharibifu: Prof. Mbarawa

Kusikiliza / Profesa Makame Mbarawa

 Mwakilishi wa Tanzaniakwenye mkutano wa IAEA kuhusu matumizi ya nguvu za atomiki Profesa Makame Mbarawa, amesema nishati hiyo inaweza kuua wadudu wanaoshambulia matunda na hivyo kuboresha soko la bidhaa hizo kimataifa.  Profesa Mbarawa ambaye ni Waziri wa mawasiliano, Sayansi na teknolojia amesema hayo katika mahojiano maalum na Radio hii kutokaAustriakunakofanyika mkutano huo.  (Sauti Mbarawa) Kadhalika [...]

18/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi kunahitaji hatua za mapema

Kusikiliza / FOREST

Shirika la mpango wa chakula duniani FAO limesema kuwa kuchukuliwa kwa hatua za mapema pamoja na uwekezaji wa kutosha ni mambo yanayohitajika ili kukabiliana na kitisho cha mabadiliko ya tabia kinachokabili misitu duniani. George Njogopa na taarifa zaidi. (Taarifa ya George) Katika taarifa yake iliyotoa mwongozo kuhusiana na uangalizi wa misitu, FAO imesema kuwa dunia inaweza [...]

18/09/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031