Nyumbani » 16/09/2013 Entries posted on “Septemba 16th, 2013”

Baraza Kuu lahitimisha kikao chake cha 67

Kusikiliza / Rais Vuk Jeremic, Kikao cha 67 cha Baraza Kuu cha hitimishwa

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo limehitimisha kikao chake cha 67, ambacho kimedumu mwaka mmoja sasa. Kuhitimishwa kwa Kikao cha 67 kunakaribisha kuanza kwa Kikao cha 68, ambacho kilele chake kitakuwa ni mkutano wa viongozi wa kimataifa mnamo wiki ijayo. Joshua Mmali ana maelezo zaidi (TAARIFA YA JOSHUA) Kikao cha 67 kiliendeshwa na Bwana [...]

16/09/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Baada ya ripoti, Baraza sasa latafakari athari na azimio laandaliwa: Rais wa Baraza

Kusikiliza / Gary Quinlan, Australia

Baada ya kupatiwa ripoti kuhusu matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria, Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa sasa linajikita katika hatua zitakazochukuliwa hususan kupitia baraza hilo, hiyo ni kauli ya Rais wa baraza hilo Balozi Gary Quinlan alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea ripoti ya uchunguzi wa matumizi ya silaha za [...]

16/09/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Sarin ilitumika Syria Je ni nani alitumia, haikuwa jukumu la Tume: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu, Ban Ki-moon

Kiwango kikubwa cha kutisha cha kemikali aina ya Sarin kilitumika kwenye shambulio la tarehe 21 Agosti huko Ghouta, kwenye viunga ya mji mkuu wa Syria, Damascus, ni kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon wakati akiwajulisha waandishi wa habari mjini New York, kile kilichomo kwenye ripoti ya uchunguzi Syria, ambayo aliwasilisha kwa [...]

16/09/2013 | Jamii: Habari za wiki, Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Monique Barbut ateuliwa kuwa katibu mkuu wa UNCCD

Kusikiliza / Monique Barbut

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kufuatia majadiliano na ofisi ya Umoja wa mataifa inayohusika na mkataba wa kukabiliana na hali ya jangwa UNCCD leo ametangaza uteuzi wa Monique Barbut wa Ufaransa kuwa katibu mkuu wa UNCCD. Bi. Barbut anachukua nafasi ya Bwana Luc Gnacadja. Ban amemshukuru bwana Gnacadja kwa mchango na kazi [...]

16/09/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Licha ya changamoto walinzi wa amani wa UM waendesha doria Sudan Kusini

Kusikiliza / Walinda amnai, UNMISS

Jimbo la Jonglei Sudan Kusini ni baadhi ya maeneo yenye changamoto zaidi kwa walinda amani kupiga doria, huku ukosefu wa usalama na hivi karibuni mvua ikiwa ni baadhi ya vikwazo basi ungana na Joseph Msami katika ripoti hii. (RIPOTI YA JOSEPH MSAMI)

16/09/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Silaha za kemikali zilitumika Syria: Ripoti

Kusikiliza / Baraza la Usalama ambalo leo limepatiwa matokeo ya ripoti ya uchunguzi huko Syria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema ripoti ya uchunguzi wa matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria tarehe 21 mwezi uliopita imethibitisha pasipo shaka kuwa silaha hizo zilitumika. Katika taarifa yake kwa Baraza la Usalama Jumatatu Ban ameelezea kusikitishwa na kiwango kikubwa cha silaha za kemikali kilichotumika na kuleta maafa kwa raia [...]

16/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IAEA yaanza mkutano mkuu wa 57 Vienna

Kusikiliza / Yukiya Amano

Zaidi ya wajumbe 2000 kutoka nchi 159 wanachama wa shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA wanakutana wiki hii mjini Vienna kwenye kituo cha kimataifa katika mkutano wa 57 wa kila mwaka wa shirika hilo. Akifungua mkutano huo wa siku tano mkurugenzi mkuu wa IAEA Yukiya Amano ameelezea mafanikio ya liyofikiwa na shirika hilo [...]

16/09/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Tume ya Pinheiro inachunguza matumizi ya silaha za kemikali Syria

Kusikiliza / Sergio Pinheiro

Baraza la Haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limejulishwa hii leo kwamba Tume ya kimataifa ya uchunguzi dhidi ya Syria inafanya uchunguzi wake huru kubaini nani anahusika na shambulio la kemikali la tarehe 21 Agosti 2013 kwenye viunga vya mji mkuu Damascus. Mwenyekiti wa Tume hiyo Sérgio Pinheiro ameeleza hayo pamoja na kile ambacho [...]

16/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Licha ya mzozo Syria, UNICEF yahakikisha watoto wanasoma

Kusikiliza / Watoto wa Syria,UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, kwa ushirikiano na wizara ya elimu na wadau wengine nchini Syria, linaunga mkono kampeni ya kuhakikisha watoto wanarejea masomoni. Kampeni hiyo inalenga watoto Milioni Moja wa shule za msingi walioathiriwa na mzozo nchini mwao. Alice Kariuki na taarifa kamili. (TAARIFA YA ALICE) Huku mwaka mpya wa [...]

16/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa idadi ya watu Asia-Pacific kuzingatia maisha bora

Kusikiliza / Mkutano wa 6 walenga maisha bora

Wajumbe wanaohudhuria mkutano wa sita wa idadi ya watu kwa Asia na Pacific wanatathimini idadi ya watu na changamoto za maendeleo zinazokabili kanda hiyo ikiwemo ongezeko la kasi la wazee, wahamiaji na mfumo wa familia. Mkutano huo unaojumuisha wajumbe kutoka nchi zote za Asia na Pacific utajadili masuala mengine yanayotoa changamoto na ambayo ni muhimu [...]

16/09/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Bodi ya UNCTAD kujadili njia mwafaka za kukabiliana na mdororo wa kiuchumi

Kusikiliza / Mkutanoni wa UNCTAD

Bodi ya usimamizi ya Kamati ya Biashara na Maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD, inakutana kujadili jinsi ya kuzisaidia nchi zinazoendelea kukabiliana na hali ya wasiwasi ilosababishwa na mdororo wa kiuchumi. Mkutano huo wa wiki mbili umeanza leo Jumatatu kwa hotuba ya Mkurugenzi Mkuu mpya wa UNCTAD, Mukhisa Kituyi. Bwana Kituyi ambaye ni raia wa [...]

16/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Homa ya mafua ya ndege bado ni tishio: FAO

Kusikiliza / Fao yaonya kuhusu homa ya mafua

Shirika la kilimo na chakula duniani, FAO limetoa taarifa mpya inayoonya kuwa homa ya mafua ya ndege aina ya H7N9 na H5N1 bado ni tishio duniani na kuitaka jumuiya ya kimataifa kuchukua tahadhari. FAO imesema kuna uwezekano virusi hao kujitokeza tena katika kipindi cha msimu wa mafua ya ndege. George Njogopa na taarifa kamili. (Taarifa [...]

16/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031