Nyumbani » 12/09/2013 Entries posted on “Septemba 12th, 2013”

Rais Bashar Al Assad asaini nyaraka za kujiunga na mkataba unaozuia silaha za kemikali

Kusikiliza / Rais Bashar Al-Assad wa Syria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon Alhamisi amepokea barua kutoka serikali ya Syria inayomtaarifu kuwa Rais Bashar Al Assad ametia saini nyaraka za kuwezesha nchi hiyo kujiunga na mkataba wa kimataifa wa kupiga marufuku uendelezaji, utengenezaji, uhifadhi na utumiaji wa silaha za kemikali wa mwaka 1992.  Msemaji wa Katibu Mkuu katika taarifa yake [...]

12/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM walaani shambulio nchini Somalia

Kusikiliza / Nicholas Kay

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Nicholas Kay amelaani vikali shambulio la gari lililokuwa limembeba kiongozi wa utawala wa mpito wa Juba Ahmad Muhammad Islam Madobe. Kiongozi huyo amenusurika na kujeruhiwa vibaya katika shambilio hilo ambapo mlinzi wake na raia mmoja wameuwawa pale gari lake lilipogongwa na gari jingine lililobeba [...]

12/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Je mtoto unaweza kuchora picha kuonyesha athari za utupaji chakula kwa mazingira duniani?

Kusikiliza / Mchoro ulioshinda mwaka huu!

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira, UNEP limeandaa shindano la kimataifa la uchoraji picha kuhusu kuokoa sayari ya dunia kwa kuepuka utupaji chakula. Shindanohilomahsusi kwa watoto wenye umri wa kati ya miaka Sita hadi 14 litafikia kilele mwakani ambapo ukomo wa kuwasilisha picha zilizochorwa ni tarehe 15 mwezi Machi mwaka 2014. Katika kuhamasisha watoto [...]

12/09/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

ICC yazungumzia mpango wa Kenya kutaka kujitoa

Kusikiliza / mwendesha mashtaka ICC

    Kesi inayaowakabili viongozi wa serikali yaKenyaakiwemo Naibu Rais William Rutto pamoja na mtangazaji wa radio Joshua Arap Sang imeanza kusikilizwa huko The Hague nchini Uholanzi.   Kesi hiyo yenye mvuto nchiniKenya, Afrika mashariki, na dunia nzima kwa ujumla inahusisha tuhuma za kuhusika na vurugu baada ya uchaguzi mkuu nchiniKenya mwaka 2007 ambapo zaidi [...]

12/09/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Tuna wasiwasi na operesheni zetu Afrika, lakini DRC kitisho cha M23 kimepungua: Ladsous

Kusikiliza / M23 Sio tishio Goma

Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani ndani ya Umoja wa Mataifa Herve Ladsous amesema wasiwasi wao mkubwa wa operesheni zao  hivi sasa uko barani Afrika hususan Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mali na Sudan. Amesema hayo mjiniNew York, Marekani wakati akitoa taarifa ya utendaji wa ofisi yake kwa waandishi kabla ya kuanza kwa mkutano [...]

12/09/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Nchi zitekeleze mkataba ili kufikia amani ya kweli DRC: UM

Kusikiliza / Gary Quinlan wa Australia

Rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Gary Quinlan ameelezea wasiwasi wa wajumbe wa barza hilo juu ya kudorora kwa amani mashariki mwa Jamhuri ya Kimdemokrasia ya Kongo, DRC na hivyo kuzitaka nchi zilizotia saini mkataba wa amani ,usalama na ushirikiano kwa ajili ya DRC na ukanda wa maziwa makuu kutekeleza ahadi zao [...]

12/09/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Vijana wataka uwazi zaidi katika uongozi

Kusikiliza / Mkutano wa vijana wang'oa nanga, Costa Rica

Vijana kutoka kila pembe ya dunia wametoa wito kwa viongozi wa wa dunia kutoa njia rahisi zaidi, za nguvu, na za wazi za masuala ya uongozi ambazo zitawafikia watu wengi zaidi kuliko za sasa. Wito huo umekuja katika azimio la vijana lililopatikana kwenye mkutano wa siku tatu wa maendeleo na teknolojia ya mawasiliano baada ya [...]

12/09/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UN-Women kuelekea ukomo wa Malengo ya milenia kuhamasisha elimu kwa mtoto wa kike

Kusikiliza / Phumzile Mlambo-Ngcuka, UN-Women

Mkurugenzi Mtendaji mpya wa shirika la umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake, UN-Women Phumzile Mlambo-Ngcuka amesema wakati ulimwengu ukijitihadi kufikia malengo ya milenia kabla ya ukomo wake mwakani, shirika lake litatumia fursa hiyo kuimarisha huduma muhimu kwa mwanamke ili kufikia lengo la ukombozi wa kundihilo. Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York, Marekani [...]

12/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Rais wa baraza kuu asisitiza suluhu ya kisiasa Syria

Kusikiliza / Vuk Jeremic (picha ya faili)

Mustakabali wa Syria ni muhimu katika usalama na ustawi wa ukanda mzima wa mashariki ya mbali na pengine dunia nzima kwa ujumla. Hiyo ni kauli ya Rais wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa Vuk Jeremic katik ataarifa yajke alioitoa leo mjini New York wakati akizungumzia mgogoro huo ambapo amesisitiza juhudi za kukomesha mapigano na [...]

12/09/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Siku ya kimataifa yaelezea faida za ushirikiano wa Kusini-Kusini:

Kusikiliza / Ushirikiano wa kusini-kusini

Alhamisi ya leo Umoja wa Mataifa unasherehekea jinsi nchi zinazoendelea zinavyotegemeana na kushirikiana utaalamu, ujuzi na taarifa katika kushughulikia matatizo kama umasikini na njaa. Siku ya Umoja wa Mataifa ya ushirikiano wa Kusini-Kusini inaadhimishwa wakati juhudi za kimataifa zikiongezeka kufikia malengo ya maendeleo ya milenia ifikapo 2015. Rebecca Grynspan, ni msimamizi mwandamizi wa shirika la [...]

12/09/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Dunia yaweza kuepuka gharama za bilioni 47 na kuokoa zingine kwa uwekezaji wa Global Fund

Kusikiliza / Nembo ya global fund

Ripoti mpya iliyotolewa Alhamisi iitwayo "Gharama za bila kuchukua hatua" inatoa changamoto kwa viongozi wa dunia kutunisha mfuko wa kimataifa kwa ajili ya kupambana na ukimwi, kifua kikuu na malaria yaani Global Fund. Flora Nducha na taarifa kamili  (TAARIFA YA FLORA NDUCHA) Maafisa wa Global Fund wamepiga mahesabu na kusema zinahitajika dola Bilioni 15 katika [...]

12/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mratibu wa masuala ya kibinadamu alaani mauaji ya watoa misaada CAR:

Kusikiliza / Bi. Kaarina Immonen akizungumza na wananchi huko Bangui

  Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) Kaarina Immonen, amelaani vikali mauaji ya wafanyakazi wawili wa misaada wa ACTED mjini Bossangoa mwishoni mwa wiki.  Bi Immonen ametoa salamu za rambirambi kwa familia na marafiki wa wafanyakazi hao na kwa wafanyakazi wote wa ambao hujitolea bila [...]

12/09/2013 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Masoko ya ndani na ya kikanda yanaweza kuchangia ukuaji wa uchumi: UNCTAD

Kusikiliza / Dr. Mukhisa Kituyi

Miaka mitano baada ya mdororo wa uchumi duniani kumalizika, bado uchumi wa dunia umesalia kuwa wenye msukosuko kwa mujibu wa ripoti kutoka kwa Shirika la biashara na maendeleo la Umoja wa Mataifa UNCTAD. Jason Nyakundi na taarifa kamili (RIPOTI YA JASON NYAKUNDI) Kupitia kwa ripoti ya kila mwaka kuhusu biashara na maendeleo UNCTAD inasema kuwa [...]

12/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Japan yaokoa wenye njaa Zimbabwe

Kusikiliza / Japan yatoa msaada kwa ajili ya Zimbabwe

Huko Zimbabwe ukosefu wa uhakika wa chakula miongoni mwa familia maskini umepata ahueni baada ya Japan kulipatia shirika la mpango wa chakula duniani, WFP dola Milioni Nne nukta Mbili kuimarisha upatikanaji wa chakula na lishe bora. Alice Kariuki anafafanua zaidi.  (RIPOTI YA ALICE KARIUKI) Msaada huo wa Japan unakuja huku kukiwa na tishio la usalama [...]

12/09/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kumiminika kwa wakimbizi Uganda, serikali yaimarisha ulinzi dhidi ya ugaidi

Kusikiliza / Wakimbizi kambini ya Hoima, Uganda

Nchini Uganda, kuendelea kumiminika kwa wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambao sasa wanahifadhiwa kwenye kambi moja huko Hoima, kumeibua wasiwasi wa uwezekano wa waasi kujipenyeza na kutishia usalama wa wakazi wa eneo hilo. Imeripotiwa kuwa polisi nchini Uganda tayari wameanza kuchukua hatua kuimarisha ulinzi kama anavyoripoti John Kibego wa radio washirika ya [...]

12/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watembea Arusha hadi Dar es Salaam kunusuru wanyamapori

Kusikiliza / Maandamano ya kupinga ujangili wa tembo yakiingia jijini Dar es salaam

Nchini Tanzania, juhudi za kukabiliana na wimbi la ujangili wa wanyamapori zimeanza kushika kasi kufuatia kampeni iliyoanzishwa na makundi ya kiharakati ambayo leo yamehitimisha safari ya kutembea kwa miguu kutoka Mkoani Arusha hadi jiji Dar es salaam. Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa zaidi ya tembo 17,000 waliuaawa katika kipindi cha mwaka 2011 na kuna uwezekano [...]

12/09/2013 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »