Nyumbani » 10/09/2013 Entries posted on “Septemba 10th, 2013”

Sababu za watu kujiua zaainishwa

Kusikiliza / Kupinga kujiua

Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kupinga vitendo vya kujiua mwandishi wa idhaa hii kutoka Nairobi Jason Nyakundi amefanya mahojiano na Dk Fredrick Owit kuhusu sababu za watu kujiua pamoja na kukusanya maoni ya wananchi jijini humo. Ungana naye katika taarifa ifuatayo yenye ufafanuzi zaidi  

10/09/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

UM wasikitishwa na Venezuela kujitoa katika mkataba wa haki za binadamu.

Kusikiliza / Rupert Colville

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu imeelezea kusikitishwa kwake na hatua ya Venezuela kujitoa katika mkataba wa haki za binadamu wa Marekani. Akiongea mjini Geneva msemaji wa ofisi hiyo Rupert Colville amesema licha ya kwamba nchi hiyo imejitoa tangu Septemba mwaka jana lakini madhara ya uamuzi huo yanaonekana leo na kusisitiza kwamba [...]

10/09/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Liberia inasonga mbele licha ya changamoto: Mkuu UNMIL

Kusikiliza / Karin Landgren, UNMIL

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo limepatiwa ripoti ya Katibu Mkuu kuhusu hali ilivyo nchini Liberia miaka kumi baada ya mlolongo wa makubaliano ya amani kutiwa saini huko Accra, Ghana. Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Liberia, UNMIL Karin Landgren amesema Liberia yapaswa kupongezwa na zaidi ya yote yahitaji usaidizi kwani [...]

10/09/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ripoti ya sauti Milioni Moja yazinduliwa, Ban asema zama mpya zataka dira mpya:

Kusikiliza / Ripoti ya Sauti ya watu millioni moja yazinduliwa

Umoja wa Mataifa leo umezindua ripoti iitwayo Sauti Milioni Moja, Dunia tuitakayo, ambayo inatokana na mkusanyiko wa maoni kutoka nchi 88 duniani kote zikijumuisha maeneo ya Afrika, Amerika Kusini na Caribbean, Asia na Pasifiki bila kusahau nchi za Kiarabu, Ulaya Mashariki na Asia ya Kati. Akizindua ripoti hiyo Katibu Mkuu Ban Ki-moon amesema malengo ya [...]

10/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Falk akaribisha uamuzi wa Uholanzi kujiondoa katika mradi haramu wa maji Israeli

Kusikiliza / Richard Falk

Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya kibinadamu  Richard Falk leo amekaribisha uamuzi uliotolewa na kampuni ya kimataifa ya Kiholanzi Royal HaskoningDHV kusitisha mkataba wake na manispaa ya Jerusalem wa kujenga kiwanda cha maji machafu Kidroni chenye lengo la kuhudumia makazi haramu ya Israeli katika Mashariki ya Jerusalemu. Kukamilika kwa mradi huo kungetoa [...]

10/09/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Misaada ya kibinadamu yafikishwa Myanmar kwa mara ya kwanza : OCHA

Kusikiliza / Misaada ya kibinadamu yafikishwa Mynmar

Ofisi ya Umoja wa kimataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA imesema magari kumi na moja yaliyoko chini ya UM na washirika wengine wa maswala ya kibiadamu yamesambaza chakula , madawa na vitu vingine kwa jamii zilizopoteza makazi huko Mynamar.Taarifa zaidi na George Njogopa (TAARIFA YA GEORGE) Hii ni mara ya kwanza katika historia ya [...]

10/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi 107 wa Syria walio Lebanon kuelekea Ujerumani Jumatano:UNHCR

Kusikiliza / Wakimbizi wa Syria walioko Lebanaon

Jumla ya wakimbizi 107 raia wa Syria wanatarajiwa kuondoka nchini Lebanon kwa makao ya muda nchini Ujerumani kupitia kwa mapngo uliotangazwa mwezi machi mwaka huu. Kundi hilo la wakimbizi linaelekea mjini Hanoverna ndilo la kwanza kupata msaada wa Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR. Wakiwasili nchini ujerumani wakimbizi hao watapelekwa  eneo la [...]

10/09/2013 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNEP yakaribisha maelewano mapya ya kuondoa gesi zinazochafua mazingira

Kusikiliza / Gesi zinazoharibu tabaka la ozone

Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP limekaribisha maafikiano kutoka kwa viongozi wa dunia kwenye mkutano wa mataifa yaliyostawi na yanayoinukia kiuchumi ya G20 mjini Moscow ya kutumika kwa mbinu mpya katika kupunguza gesi zinazochafua mazingira zinazojulikana kama hydrofluorocarbons. Alice Kariuki na taarifa kamili  (TAARIFA YA ALICE KARIUKI) Serikali kutoka nchi 25 na Jumuiya [...]

10/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mizozo kugharimu masomo ya mamilioni ya watoto duniani kote: Zerougui

Kusikiliza / Mtoto shuleni

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya watoto na mizozo ya kivita, Leila Zerrougui amesema mizozo inayoendelea maeneo mbali mbali duniani inasababisha mamilioni ya watoto washindwe kwenda shule kuhudhuria masomo, jambo ambalo ni haki yao ya msingi. Ripoti ya Grace Kaneiya inafafanua zaidi. (Ripoti ya Grace) Mbele ya kikao cha [...]

10/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Saudia imechanga dola milioni 10 kwa wakimbizi wa Kipalestina kutoka Syria

Kusikiliza / Nembo ya UNRWA

Ufalme wa Saudia umeitika wito wa ombi la Syria la msaada kwa ajili ya shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA na kutoa dola milioni 10 kupitia mfuko wa Saudia kwa maendeleo. Machafuko nchini Syria yanaendelea kuathiri kambi za UNRWA ambayo inakadiria kwamba zaidi ya nusu ya wakimbizi 529,000 wa [...]

10/09/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

William Ruto na Joshua Arap Sang wakana mashtaka dhidi yao huko The Hague

Kusikiliza / William Ruto akiwa mahakamani The Hague

Huko The Hague hii leo imeanza kusikilizwa kesi dhidi ya William Ruto, Naibu Rais wa Kenya na Joshua Arap Sang, mwandishi wa habari wa kituo kimoja cha Radio. Mbele ya jopo la majaji watatu linaloongozwa na  Jaji Chile Eboe-Osuji kutokaNigeria, William Ruto na Joshua arap Sang walisomewa mashtaka dhidi yao na mwendesha mashtaka Anton Stynberg.  (Sauti [...]

10/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mgogoro wa Syria umeacha makovu yasiyoonekana kwa watoto:UNICEF

Kusikiliza / Watoto nchini Syria

Kuendelea kushuhudia vita  na machafuko kwa muda mrefu, kutawanywa, kupoteza rafiki zao na familia za na pia kuzorota kwa hali ya maisha kumewaacha watoto wa Syria na makovu ya daiama limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. Kwa mujibu wa mkurugenzi wa UNICEF kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika Maria Calivis [...]

10/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031