Nyumbani » 09/09/2013 Entries posted on “Septemba 9th, 2013”

Ban na Malkia Sofia wa Hispania wazungumzia masuala ya ulemavu na Syria

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon na Malkia Sophia wa Hispania

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amekuwa na mazungumzo na Malkia Sofia wa Hispania mjini New York, ambako amekuja kwa ajili ya kupokea tuzo maalum ya nchi yake kuhusu harakati za kusaidia watu wenye ulemavu. Katika mazungumzo yao wamejadili mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu ulemavu [...]

09/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Itakuwa vyema Syria ikikabidhi silaha zake za kemikali: Ban

Kusikiliza / SG Ban Ki-moon

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema pendekezo la Urusi kwa Syria kuweka silaha zake za kemikali chini ya uangalizi wa kimataifa ni zuri na kwamba iwapo Syria itakubali, jumuiya ya kimataifa itachukua hatua haraka kutekeleza mpango huo. Bwana Ban amesema hayo wakati akijibu swali la waandishi wa habari mjini New York, [...]

09/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Biashara zaimarika Somalia

Kusikiliza / Barabara Somalia

Barabara za Mogadishu zilijulikana kama hatari zaidi kote duniani, zilkuwa ni mahali ambako kulishudiwa ghasia siku nenda siku rudi lakini nyakati zimebadilika na hali imebadailkia pia kwani sasa biashara zinaweza kuendeshwa hapa basi ili kujua hali ilivyo Mogadishu ungana na Joseph Msami  

09/09/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Uwekezaji unakwamishwa na uchumi na sera dhaifu- Mkuu UNCTAD

Kusikiliza / Mikhisa Kituyi

Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la biashara na maendeleo UNCTAD, Mukhisa Kituyi ameonya kwamba mpango wa wa kufufua uwekezaji kimataifa unasuasua kufuatia wawekezaji kusita kupanua biashara katika wigo wa uchumi unaolegalega na kutokuwa na uhakik wa sera. Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya baraza hilo kuhusu uwekezaji Akizungumza katika kongamano la 17 [...]

09/09/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM wakaribisha mipango ya kitaifa kupinga ubaguzi wa rangi Mauritania:

Kusikiliza / Mutuma Rutere

  Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ubaguzi wa rangi Mutuma Ruteere, amepongeza hatua ya serikali ya Mauritania ya kuanza mchakato wa kuandaa mipango ya hatua za kitaifa dhidi ya ubaguzi wa rangi , lakini ameitaka nchi hiyo kuchambua na kutathimini vipengele vyote vya ubaguzi. Alice Kariuki na taarifa kamili. Bwana Ruteere akihitimisha ziara [...]

09/09/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa kipalestina wapata makazi mapya bora huko Gaza

Kusikiliza / Wakimbi wa Kipalestina

Zaidi ya wakimbizi 1,200 wa kipalestina wanaoishi Gaza, wamekabidhiwa makazi mapya kwenye eneo la Khan Younis, kufuatia kukamilika kwa mradi wa ujenzi kwenye ukanda wa Gaza,. Mradi huo wa makazi mapya 226 umetekelezwa na Japani kwa ushirikiano na shirika la Umoja wa Mataifa la kusaidia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA. Mkuu wa operesheni wa UNRWA Robert [...]

09/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatua za kijeshi zinawaweza kuchokea hali kuwa mbaya Syria:Pillay

Kusikiliza / Navi Pillay

Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema hatua za kijeshi kutoka nje au kuyapa silaha makundi ya waasi haiwezi kuleta amani nchini Syria.Jason Nyakundi anaaarifu (PKG YA JASON NYAKUNDI) Akihutubia baraza la haki za binmadamu la Umoja wa Mataifa Pillay amesema kuwa mateso wanayopitia wananchi wa Syria yamefikia viwango vya [...]

09/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mipango ya nyuklia ya DPRK na IRAN yatutia hofu: Mkuu IAEA

Kusikiliza / Yukiya Amano

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la nishati ya atomiki duniani, IAEA, Yukia Amano amesema bado ana wasiwasi mkubwa na mipango ya nyuklia ya Korea Kaskazini-DPRK na Iran. Amano ameieleza bodi ya magavana wa shirika hilo Jumatatu kuwa wasiwasi wake kuhusu Korea Kaskazini unatokana na taarifa za nchi hiyo kuhusu jaribio la tatu la nyuklia, nia yake [...]

09/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Yaya Toure apeperusha bendera kuokoa Tembo wa Afrika

Kusikiliza / Balozi mwema Yaya Toure

Balozi mwema wa shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira, UNEP ambaye pia ni mwanasoka nyota ulimwenguni kutoka Cote d'Ivoire, Yaya Toure ametumia mechi ya kusaka kufuzu kucheza kombe la dunia kati ya timu yake ya Taifa na ile ya Morocco kutuma ujumbe thabiti dhidi ya ujangili wa tembo barani Afrika. George Njogopa na taarifa [...]

09/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

INTOSAI sasa kukagua utekelezaji wa mikataba ya kuhifadhi mazingira

Kusikiliza / UNEP_logo-298x300

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mazingira UNEP limetiliana saini na chombo cha kimataifa cha ukaguzi, INTOSAI kwa ajili ya kufuatilia utekelezaji wa mikataba 280 inayohusu mazingira ambayo ilisainiwa katika siku zilizopita. Mikataba hiyo ni pamoja na ile inayohusu mabadiliko ya tabia nchi,taka hatarishi na maeneo mengine yanyohusu dunia kwa ujumla. Makubaliano hayo ambayo [...]

09/09/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031