Nyumbani » 04/09/2013 Entries posted on “Septemba 4th, 2013”

Bado kuna mkwamo ndani ya Baraza la usalama kuhusu Syria: Balozi Quinland

Kusikiliza / Rais wa Baraza la Usalama kwa mwezi Septemba, Balozi Gary Quinlan wa Australia

Mpango kazi wa mwezi Septemba kwa Baraza la usalama la Umoja wa mataifa chini ya uongozi wa Australia umeonyesha kuwa suala la Mashariki ya Kati hususan Syria litaendelea kuangaziwa. Mpango kazi huo umewasilishwa kwa waandishi wa habari na Mwakilishi wa kudumu waAustraliakwenye umoja wa mataifa Balozi Gary Quinlan. Amesema kadri siku zinavyosonga watu wengi wanashangaa [...]

04/09/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa Syria waendelea kumiminika Lebanon

Kusikiliza / Wakimbizi wa Syria walioko Lebanon

Dunia hivi sasa inaelekeza macho yake nchini Syria nchi ambayo mzozo unaoendelea umesababisha madhila kwa raia wa nchi hiyo ikiwamo kuwa wakimbizi. Raia wa nchi hiyo wamejikuta wakimbizi katika nchi za jirani mathalani Iraq, Uturuki na kwingineko. Lakini hali ni mbaya zaidi nchini Lebanon ambapo lundo la wakimbizi wako nchini humo. Ungana basi na Grace [...]

04/09/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Nchi zinazohifadhi wakimbizi na UNHCR kujadili mgogoro wa Syria

Kusikiliza / Wakimbizi wa Syria wamiminika katika maeneo ya mpaka, Iraq

Mawaziri wa nchi kutoka Iraq, Jordan, Lebanon na Uturuki  wanakutana mjini Geneva leo Jumatano kushiriki mkutano kuhusu matatizo ya wakimbizi wa Syria, mkutano unaongozwa na kamishina mkuu wa wakimbizi António Guterres. Mkutano huo unafanyika siku moja baada ya idadi ya Wasyria walioorodheshwa kama wakimbizi au wanaosubiri kuorodheshwa imepindukia milioni 2, na Shirika la kuhudumia wakimbizi [...]

04/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya usalama wa chakula ukanda wa Sahel bado mbaya:FAO

Kusikiliza / Eneo la Sahel bado linashuhudia mzozo wa chakula

Takribani wakazi Milioni Kumi na Mmoja katika ukanda wa Sahel bado hawana uhakika wa chakula, hiyo ni taarifa ya shirika la chakula na kilimo duniani, FAO iliyotolewa leo ikiwa ni tahadhari wakati huu ambapo familia zimetumia akiba yote ya chakula huku zikikabiliwa na bei ya juu za vyakula wakati wakisubiria msimu ujao wa mavuno. Ripoti [...]

04/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wavamizi wa eneo la wakimbizi huko Uganda wafurushwa

Kusikiliza / Wanaofurushwa, Uganda

Serikali ya Uganda imeanza kuwafurusha zaidi ya watu elfu hamsini walioingilia ardhi ya Kambi ya wakimbizi ya Kyangwali. Zoezi hilo lina lengo la kupata makazi kwa maelfu wakimbizi ya wanaoendelea kuingia nchini humo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia Congo (DRC). John Kibego wa radio washirika ya Spice FM, anaripoti kutoka Hoima, Uganda. (Tarifa ya Kibego) Wanofurushwa [...]

04/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bado nasisitiza suluhisho la kisiasa kwa mgogoro wa Syria: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-Moon akitoa mhadhara kwenye Chuo Kikuu cha St. Petersburg, Urusi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ambaye yuko ziarani barani Ulaya, ametoa mhadhara kwenye Chuo Kikuu cha St. Petersburg nchini Urusi na kusema kuwa yeye bado anaendelea kusisitiza suluhisho la kisiasa kwa mzozo wa Syria. Ripoti ya Assumpta Massoi inafafanua zaid. (Ripoti ya Assumpta) Mhadhara wa Katibu Mkuu kwa wanafunzi wa chuo hicho [...]

04/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mabilioni ya watu bado wameachwa nyuma katika jamii ya kidigital:PGA

Kusikiliza / Vuk Jeremic

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa amesema hivi sasa 1/5 ya nyumba zote katika mataifa yanayoendelea zimeunganishwa na mtandao wa internet hii ikiwa ni ongezeko la asilimia 13 ikilinganishwa na miaka mitatu iliyopita. Bwana Vuk Jeremic ameyasema hayo jumatano kwenye mjadala maalumu kuhusu uboreshaji wa kunganishwa na mtandao Eurasia. Hata hivyo amesema ingawa [...]

04/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mabomu mtawanyiko yatumika nchini Syria

Kusikiliza / syria-shell-300x257

Wakati madai ya matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria yakiwa yanachunguzwa, hii leo kundi la kimataifa linalofanya kampeni ya kupiga vita mabomu ya kutegwa ardhini limechapisha ripoti inayodai kuwa jeshi la Syria linatumia kwa kiasi kikubwa mabomu mtawanyiko kwenye maeneo ya raia. Ripoti ya George Njogopa inafafanua zaidi. (PKG YA GEORGE NJOGOPA) Ripoti hiyo [...]

04/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hofu ya usalama wa Taifa kamwe isiwe halalisho la kutisha waandishi wa habari

Kusikiliza / Frank la Rue

Wataalamu wawili huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya kujieleza na udhibiti wa ugaidi wametaka maelezo zaidi kutoka serikali ya Uingereza kufuatia tukio la hivi karibuni la mwandishi wa habari David Miranda, mshirika mwa mwandishi Glenn Greewald wa gazeti la Guardian kushikiliwa kwa saa kadha kwenye uwanja wa ndege wa Heathrow na vifaa vyake [...]

04/09/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban awataka watu wa Maldives kuendesha uchaguzi ujao kwa amani na utulivu:

Kusikiliza / KM Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewataka watu wa Maldives kuhakikisha kwamba uchaguzi ujao wa Rais hapo Septemba 7 unafanyika kwa njia inayostahili na kwa amani. Katika uchaguzi huo Ban amewachagiza wagombea wote wa Urais kuheshimu matokeo ya uchaguzi bila kujali nani ameshinda na amewataka wadau wote kumaliza tofauti zao. Katibu Mkuu pia [...]

04/09/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031