Nyumbani » 03/09/2013 Entries posted on “Septemba 3rd, 2013”

Shambulio lolote dhidi ya Syria bila idhini ya Baraza la Usalama ni batili: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amekutana na waandishi wa habari mjini New York, Marekani hii leo ambapo suala kuu lilikuwa ni kutoa taarifa kuhusu hatua zilizofikiwa za uchunguzi wa silaha za kemikali zinazodaiwa kutumika kwenye eneo la Ghouta, nchiniSyriawiki mbili zilizopita. Ripoti ya Assumpta Massoi inafafanua zaidi.  (Taarifa ya Assumpta)  Mkutano huo [...]

03/09/2013 | Jamii: Habari za wiki, Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

UNICEF yahaha kuhakikisha watoto Syria wanasoma, licha ya machafuko.

Kusikiliza / Watoto shuleni chini ya Unicef

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linahaha kuhakikisha watoto walioathiriwa na machafuko nchini Syria wanapata elimu bila kujali ikiwa machafuko yataendelea katika siku za usoni au la. Akiongea mjini Geneva msemaji wa UNICEF Marxie Mercado amesema watoto milioni 1.9 waliokuwa darasa la kwanza hadi la tisa waliacha shule katika mwaka wa masomo [...]

03/09/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Naibu Katibu Mkuu wa UM asisitiza umuhimu wa kushughulikia masuala ya usafi:

Kusikiliza / Jan Eliasson

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson amesisitiza umuhimu wa kushughulikia masuala ya usafi na kujisaidia hadharani. Bwana Eliasson ameyasema hayo mjini Stockholm, Sweden ambako mamia ya wajumbe kutoka kote duniani wanakutana katika wiki ya maji duniani. Akitoa ujumbe maalumu kwa wiki hii chini ya kauli mbiu "kujenga ushirikiano kwa ajili ya usafi [...]

03/09/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Michezo yatumika kupinga ulemavu Bosnia

Kusikiliza / michezo ikipinga ulemavu

  Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, kwa kushirikiana na washirika wanafanya kampeni maalum ya kupambana na ulemavu kwa watoto kwa kutumia michezo ili kuifikia jamii.  Kampeni hii inayowahusisha watoto inalenga kubadilisha mtizamo wa jamii kuhusu watoto wanaosihi na ulemavu ili kuwajumuisha katika kila nyanja kwenye jamii.    

03/09/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa Syria walioko Lebanon wapatiwa hifadhi Ujerumani

Kusikiliza / Wakimbizi wa Syria walioko Lebanon

Wakati mapigano nchini Syria yakizidi kupamba moto Serikali ya Ujerumani imekubali kuwapatia ukazi wa muda raia elfu tano wa Syria wanaoishi Lebanon, na hiyo ni kwa mujibu wa shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM. Patrick Maigua amefanya mahojaino na Msemaji wa IOM Jumbe Omari Jumbe kufahamu undani wa mchakato wa kuwapeleka wakimbizi hao wa Syria [...]

03/09/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Kesi ya Trayvon:Watalaam wa UM waitaka Marekani kukamilisha haraka uchunguzi wake

Kusikiliza / unlogo1blue

Jopo la wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanaoangazia watu wa asili ya Kiafrika wameitaka Marekani kukamilisha bila kuchelewa upitiwaji wa kesi ikiwemo mauwaji ya Trayvon Martin yaliyotokea February mwaka 2012. Jopo hilo limetaka pia kutolewa kwa hukumu ya haki itakayokwenda sambamba na fidia kwa waathirika. Idara ya Mahakama kwa kushirikiana na ofisi ya mwanasheria mkuu [...]

03/09/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ujumbe wa UNAMI washuhudia hali halisi kambi ya Ashraf

Kusikiliza / Kambi ya Ashraf iliyoko nchini Iraq

Ziara ya ujumbe wa ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Iraq, UNAMI kwenye kambi ya Ashraf iliyokumbwa na mauaji mwishoni mwa wiki, imewezesha kupata picha halisi ya kile kilichotokea na hatimaye wakazi wa eneohilokuruhusu maiti zilizokuwa zimehifadhiwa eneohilokwa muda kusafirishwa hadi Baquba. Ujumbe huo uliongozwa na naibu mwakilishi maalum wa katibu Mkuu wa Umoja wa [...]

03/09/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mtalamu huru wa UM asifu mwelekeo wa haki za binadamu Somalia

Kusikiliza / Shamshul Bari

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini Somalia Shamsul Bari amepongeza kupitishwa kwa mpango wa utekelezaji na usimamizi wa haki za binadamu nchini humo. Bari amesema kitendo hicho cha serikali ya Somali kinaweka msingi wa kuimarisha uendelezaji na ulinzi wa haki za binadamu. haki za binadamu. Hata hivyo ametaka serikali kupanua [...]

03/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya chakula nchini Zimbabwe yazidi kuzorota: WFP

Kusikiliza / WFP ZIMBABWE

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP linasema zaidi ya watu Milioni Mbili nchini Zimbabwe wanakabiliwa na uhaba wa chakula. Grace Kaneiya na ripoti kamili. (Taarifa ya Grace) Katika kukabiliana na hali hiyo ya uhaba wa chakula Zimbambwe, WFP na washirika wake watagawa nafaka pamoja na mafuta ya kupikia. Pia mgao wa fedha utatolewa kwenye [...]

03/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ujerumani yawapatia wasyria Elfu Tano makazi ya muda: IOM

Kusikiliza / unhcr-syrian-refugees-lebanon

Serikali ya Ujerumani imekubali kuwapatia ukazi wa muda raia elfu Tano wa Syria wanaoishi Lebanon, na hiyo ni kwa mujibu wa shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM. Wakimbizi hao wametambuliwa na UNHCR na watasafirishwa kwa ndege maalum zilizokodishwa na IOM kutoka Beirut kwenda Hanover Ujerumani katika kipindi cha mwaka mmoja. Tayari IOM imeaanza kutoa mafunzo [...]

03/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu 75,000 wakosa makazi Sudan Kusini

Kusikiliza / Sudan Ocha

Mashirika ya kutoa misaada nchini Sudan Kusini yanasema kuwa hadi sasa yameandikisha kiasi cha watu 75,000 walioathiriwa na machafuko katika jimbo la Jonglei.  Mashirika hayo yameanza kutoa huduma za usamaria wema ikiwemo usambazaji wa vyakula, maji pamoja na huduma nyingine za usafi. (TAARIFA YA ALICE KARIUKI) Shughuli za usambazaji wa misaada hiyo imeanza kwa kasi [...]

03/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yasema idadi ya wakimbizi wa Syria yafikia milioni mbili

Kusikiliza / Syrians-Iraq-12-300x257

Idadi ya wakimbizi wa Syria inaripotiwa kufikia milioni mbili wakati nchini Syria kwenye hali ikizidi kuwa mbaya kwa kuzalisha wakimbizi wa ndani. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema kuwa hadi nchini Syria kwenyewe kuna zaidi ya wakimbizi 4.25. George Njogopa na maelezo kamili: (PKG YA GEORGE NJOGOPA) Kwa mujibu wa shirika [...]

03/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ofisi ya haki za binadamu yalaani vikali shambulio la Asharaf Iraq:

Cécile Pouilly, Msemaji wa Ofisi ya Tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imelaani vikali shambulio dhidi ya kambi ya Asharaf nchini Iraq siku ya Jumapili. Katika shambulio hilo wakaazi 47 wa kambi hiyo waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa. Ofisi ya haki za binadamu imeitaka serikali ya Iraq kuhakikisha ulinzi na usalama kwa wakazi wa kambi hiyo na kufanya uchunguzi [...]

03/09/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF inasaidia watoto walioathirika na vita Mali

Kusikiliza / Mwalimu akiwa darasani nchini Mali

Nchini Mali, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linaongeza juhudi zake za kusaidia watoto nusu milioni ambao maisha yao yameathirika na vita, mafuriko na ukosefu wa lishe ili waweze kurejea shuleni. Karibu shule 200 zimefungwa, kuharibiwa au kuporwa na sehemu zingine zimezingirwa na mabomu ambayo hayajalipuka kufuatia waasi nchini humo kuliteka eneo [...]

03/09/2013 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031