Zaidi ya Wairaq 1000 wameuawa mwezi Julai:UNAMI

Kusikiliza /

 

Takwimu za maafa na majeruhi ya wairaq imetolewa:UNAMI

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa leo na mpango wa Umoja wa mataifa nchini Iraq UNAMI , jumla ya Wairaq 1057 wameuawa  na wengine 2326 kujeruhiwa katika vitendo vya kigaidi na ghasia kwa mwezi wa Julai.Wengi waliopoteza maisha ni raia ambao ni jumla ya 928 huku polisi 204 nao wakiaga dunia.Kwa upande wa majeruhi raia ni 2109 wamejeruhiwa na polisi 338. Kwa upande wa majeshi ya ulinzi na usalama UNAMI inasema jeshi la Iraq limepoteza askari 129 na kuwaacha wengine 217 wakiwa wamejeruhiwa.

Akionya kuhusu machafuko nchini humo kaimu mwakilishi wa Umoja wa mataifa Gyrogy Busztin amesema athari za machafuko kwa raia zinasalia kuwa za juu kwani tangu mwanzoni mwa mwaka huu raia 4137 wameuawa na wengine 9865 wamejeruhiwa.

Baghdad ndio iliyoathirika zaidi ikifuatiwa na Salahuddin, Ninewa, Diyala, Kirkukand Anbar , huku miji ya Babil, Wasit na Basra nayo ikiarifu kuhusu vifo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031