WFP inahitaji dola milioni 30 kila wiki kuendesha oparesheni zake nchini Syria

Kusikiliza /

WFP inatoa msaada Syria(picha ya WFP-Eman Mohammed)

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linasema kuwa mwezi uliopita wa Julai lilifanikiwa kuwafikia karibu watu milioni 2.9 walioathiriwa na mzozo unaondelea nchiniSyria. Mwezi huu wa Agosti WFP ilikuwa na mpango wa kufikia wakimbizi milioni tatu. Wakimbizi milioni 1.1 kwenye nchi majirani walipata msaaada wa chakula kutoka WFP lakini  hata hivyo Shirika hilo linasema kuwa oparesheni zake nchini Syria zianakabiliwa na uhaba wa dola milioni 607 huku likihitaji kuchangisha dola milioni 30 linazohitaji kila wiki kuhahudmia wale walioathiriwa na mzozo. Elizabeth Byrs ni msemaji wa WFP.

 (SAUTI YA ELIZABETH)

"Kwa hiyo Shirika la mpango wa chakula duniani linahitaji dola Milioni 30 Kila wiki kwa ajili ya operesheni zake ndani na nje ya Syria, ili kuweza kujaribu kupeleka misaada ya vyakula ndani na nje ya Syria."

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031