Wawili wabainika kuwa na virusi vya homa ya Corona huko Qatar: WHO

Kusikiliza /

Mtaalamu kwenye maabara

Shirika la afya duniani, WHO limesema watu wawili wamethibitishwa kuwa na uambukizo wa kirusi cha homa yaCorona, MERS-CoV, nchiniQatar. Watu hao ni wanaume wawili mmoja mwenye umri wa miaka 59 na mwingine miaka 29. Mgonjwa wa kwanza alisafiri hadi Medina Saudi Arabia kwa siku sita na kurejeaQatarilhali mwingine kumbukumbu hazionyeshi kuwa alisafiri nje ya nchi hivi karibuni.Wagonjwa wote wako hospitali hali zao ni nzuri na imeelezwa kuwa uthibitisho wa uambukizo huo ulitolewa na maabara ya kimataifa. Uchunguzi wa virusi hivyo kwa watu 138 nchiniQatarumeonyesha hawajaambukizwa. WHO imesema kwa sasa haishauri uchunguzi maalum kwa wasafiri wala kizuizi cha biashara au safari kutokana na ripoti za wagonjwa wapya. Tangu mwezi Septemba mwaka jana watu 104 duniani wamethibitishwa kuambukizwa kirusi hicho cha homa yaCoronana katiyao49 wamefariki dunia.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031