Watu milioni 770 bado wanaupungufu wa vyanzo bora vya maji:UNDP

Kusikiliza /

 

Upatikanaji wa maji safi na salama bado changamoto:UNDP

Maji ndio kitovu cha machafuko ya kila siku yanayowakabili mamilioni ya watu duniani, yakitishia maisha, amani na usalama wa watu amesema afisa msaidizi wa shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo UNDP Rebecca Greenspan.

Bi Greenspan ameyasema hayo kwenye mkutano wa kimataifa wa ngazi ya juu kuhusu ushirikiano wa maji unaoendelea huko Dushambe, Tajikistan ambako ameongeza kuwa watu takribani milioni 770 duniani kote bado wanakabiliwa na upungufu wa vyanzo bora vya maji na wengine  bilioni 2.5 wanapungukiwa na fursa ya vifaa muhimu vya usafi.

Kwa mujibu wa Bi Greenspan, amesema sio tuu kwamba dunia inakabiliwa na ongezeko la mahitaji ya maji , lakini pia ongezeko la maji taka na uchafuzi wa maji vinatishia uslama wa maji hayo na mfumo wa maisha ya viumbe masuala ambayo ni muhimu kwa maisha na usaslama wa chakula.

Amesema mabadiliko ya hali ya hewa pia hayasaidii katika suala la upatikanaji wa maji na matukio mengine kama mafuriko na ukame unafanya hali ambayo tayari ni mbaya kuwa mbaya zaidi. Amesema endapo hali hii itaendelea basi ifikapo 2025 watu takribani bilioni 3 watakuwa wanaishi katika maeneo yenye ukwasi wa maji.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031