Wataalamu wa UM walaani utumiaji wa silaha za kemikali nchini Iraq

Kusikiliza /

Adama Dieng

Wajumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na uzuaji wa uzuiaji wa mauwaji ya halaiki na yule anayehusika na wajibu wa kuwalinda raia, wamelaani vikali mauwaji ya mamia ya raia yaliyotokea katika vitongoji vya mji wa Damascus nchini Syria mwishoni mwa wiki.

Bwana. Adama Dieng, na Bi Jennifer Welsh, wametaka kufanyika uchunguzi juu ya mauwaji hayo na wameelezea haja ya kuruhusiwa kwa wakaguzi wa Umoja wa Mataifa nafasi ya uchunguzi dhidi ya madai ya kutumika kwa silaha za kemikali. Taarifa zaidi na Alice Kariuki

(Taarifa ya Alice)

Wataalamu hao wawili wamesema kuwa matumizi ya silaha za kemikali katika mzozo huo ni kosa linalokwenda kinyume na sheria za kimataifa na wametaka pande zote kutambuahilo.

Wamesema kuwa, matumizi ya silaha ya iana hiyo kwenye maeneo yanayokumbwa na migogoro hayaruhusiwa kwani kwa kufanya hivyo ni kukiuka mkataba wa uliopitishwa mwaka 2005 na jumuiya ya kimataifa.

Walipokutana kwa mara ya kwanza kwenye kongamano la kimataifa lilolofanyika mwaka 2005, wakuu wan chi walikubaliana kwa pamoja kupitisha azimio la kuwalinda raia dhidi ya uhalifu wowote wa kivita.

Kwa upande mwingine wataalamu hao wameitaka serikali ya Syria kuwapa kibali kisicho na masharti wakaguzi wa Umoja wa Mataifa kutembelea maaeneo ambayo mauwaji hayo yametokea na kukusanya taarifa za ushahidi.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930