Wataalamu wa UM kukutana Geneva kujadilia mwongozo mpya wa haki za binadamu

Kusikiliza /

Bendera ya Umoja wa Mataifa

Jopo la wataalamu wa Umoja wa Mataifa linalohusika na kukabiliana na mwenendo wa kuwatia watu kuzuizini kiholela, litakutana Geneva, Uswisi kwa ajili ya kuandaa mwongozo ambao utatumika kwenye vyombo vya mahakama wakati inaposikiliza kesi za kukabiliana na hali ya kukamata watu ovyo ovyo.

Mmoja wa maafisa wa jopo hilo El Hadji Malick Sow amesema kuwa misingi hiyo itakayowekwa itatoa mwongozo kwa nchi wanachama kuachana na tabia ya kuwaandama raia wake.

Jopo hilo lilianzishwa kupitia azimio lililopitishwa na Baraza la Usalama mwaka 2002 ambalo lilitoa mamlaka baraza la haki za binadamu kuunda chombo kitakachomulika na kufuatilia haki za raia.

Jopo hilo linaundwa na wataalamu kutoka makundi mbalimbali ikiwemo wale wanaotoka serikalini na wale kutoka taasisi za kiraia.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2017
T N T K J M P
« apr    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031