Wataalamu wa haki za binadamu wataka kusitishwa kwa ghasia nchini Misri

Kusikiliza /

Kundi la wataalamu wa masuala ya haki za binadamu kutoka Umoja wa Mataifa wametaka kusitishwa mara moja kwa ghasia ambazo zimesababisha vifo vingi pamoja na majejeraha mjini Cairo nchini Misri siku za hivi majuzi. Wataalamu hao wameshutumu kile ambacho wamekitaja kuwa matumizi ya nguvu kupita kiasi kutoka kwa vikosi vyta usalama wakisema kuwa maandano ya amani hayastahili kuzimwa kwa kutumia nguvu.

Wametaka wale waliohusika kwenye mauaji na ukikaji mwingine wa haki abinadamu kuwajibikia vitendo vyao pamoja na sheria ya kimataifa. Wataalamu hao walilezea wasiwasi wao kutokana na idadi ya wale waliokufa wakiwemo wanawake , vijana na waandishi wa habari idadi hiyo ikiripitiwa kuzidi watu 600 kutokana na ghasia za siku ya Jumatano ambapo wanajeshi walichukua hatua ya kuvunja maandamano katikati mwa mji wa Cairo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2017
T N T K J M P
« sep    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031