Wakimbizi wa DRC wapata ajali huko Uganda, mmoja afariki dunia

Kusikiliza /

Wakimbizi wa DRC

Mtoto mmoja amefariki dunia na watu wengine 24 wamejeruhiwa baada ya basi iliyokuwa ikisafirisha wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kupinduka huko Uganda. John Kibego anaripoti kutoka Hoima, Uganda.

(Taarifa ya Kibego)

Wakimbizi hao walikuwa wakisafirishwa kutoka kambi ya wakimbizi ya Bubukwanga wilayani Bundibugyo kwelekea Hoima katika Kambi ya Wakimbizi ya Kyangwali. Huyo ni mmjoja wa majeruhi akiongea dakika chache bada ya kufikishwa kwenye hospitali ya Kagadi. Shirika la Umoja wa Mataifa Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) linagharamia mahitaji yote ya wakimbizi hao wakiwa hospitalini, likishirikiana na shirika la MSF. Alice Rutunya ni Mkuu wa ofisi ya UNHCR wilayani Hoima.

(Sauti ya Alice Rutunya)

Wakimbizi hao ni sehemu ya zaidi ya watu 20,000 waliotoroka mapigano kati ya jeshi la serikali ya Jamhuri ya Kidemukrasia ya Congo na makundi yenye bunduki katika mji wa Kamango mwezi uliopita.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2017
T N T K J M P
« apr    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031