Utoaji wa chakula shuleni waimarisha elimu, afya na kipato.

Kusikiliza /

Mpango wa lishe shuleni una manufaa:FAO

Utafiti ulioendeshwa na Shirika la chakula na kilimo, FAO unaonyesha kwamba mpango wa kuwalisha chakula wanafunzi mashuleni unaongeza ulinzi wa kijamii, chakula na lishe kwa wanafunzi.

Utafiti huo ulioangazia utaoaji wa chakula mashuleni na uwezekano wa kununua nafaka moja kwa moja kutoka kwa familia husika umehusisha nchi nane ambazo ni Bolivia, Colombia, El Salvador, Guatemala, Honduras, Nicaragua, Paraguay na Peru na unaonyesha kwamba mpango huo unaimarisha mahudhurio na kukuza mchakato wa kujifunza.

Mkurugenzi Mkuu wa FAO , José Graziano da Silva amesema mbinu hiyo ina faida tatu alizoziainisha kwamba ni usalama wa ubora wa chakula kwa wanafunzi katika shule za uma, kukuza matumizi ya chakula chenye afya na safi pamoja na kufungua uwezekano wa masoko na kipato kikubwa kwa wakulima huku ukikuza maendeleo ya maeneo husika.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031