Unyonyeshaji mtoto hupunguza uwezekano wa mama kupata saratani ya titi:UNICEF

Kusikiliza /

Mtoto akinyonya

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Tanzania limetumia kilele cha wiki ya unyonyeshaji duniani kuelezea faida anazopata mama iwapo ataamua kuanza kumnyonyesha mtoto wake punde tu baada ya kujifungua.

Mwakilishi wa UNICEF katika sherehe za kilele hicho zilizofanyika mjini Dar es salaam, Tanzania Dokta Jamal Malaga ametaja faida hizo kuwa ni pamoja na uwezekano mdogo wa kupata msongo wa mwanzo wa mawazo baada ya kujifungua, saratani ya titi pamoja na kinga dhidi ya maradhi ya unene kupita kiasi kwa mtoto aliyejifungua pamoja na maziwa ya mama kama tunu kwa mtoto.

(SAUTI YA Dokta Malaga)

Makala kamili kuhusu kilele cha wiki ya unyonyeshaji katika nchi za maziwa makuu ya Afrika itakujia siku ya Alhamis

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2017
T N T K J M P
« jun    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
31