UNEP kuangazia mchango wa jamii za asili kuelekea kwenye uchumi usioathiri mazingira

Kusikiliza /

Achim Steiner

Katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya jamii za asili Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa limeangazia mchango unaotoka kwa jamii za kiasili ambazo sasa zinawakilisha asilia tano ya watu wote dunaini katika kutimiza maendeleo endelevu. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Mkurugenzi mkuu wa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP Achim Steiner anasema kuwa kupitia kwa njia zisizo na madhara za kuhifadhi chakula na usimamizi kwenye maeneo ya mbuga jamii za asili zinatoa mchango mkubwa katika jitihada za kuhakisha kuwepo kwa uchumi usioathiri mazingira. UNEP ina lengo la kuyapigia darubini masuala ya jamii za asili katika usimamizi wa mazingira kupitia kwa teknolojia zenye gharama ya chini na njia za kuzuia kuharibika kwa mazingira. Siku ya kimataifa ya jamii za asili ya mwaka huu itaangazia zaidi kujumuishwa kwa jamii hizo katika kutunza sera ambapo pia mafanikio ya jamii hizo katika maendeleo endelevu yataangaziwa. Ikiwa ni sehemu ya siku ya mazingira duniani ya mwka huu Shirika la UNEP limeangazia njia za kitamaduni zinazotumiwa na jamii za asili kote duniani katika kuzuia kutupwa kwa chakula.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29