UM watilia shaka ustawi wa watoto walioko kwenye makambi nchini Syria

Kusikiliza /

Watoto kambini

Umoja wa Mataifa umesema kuwa makambi mengi yanayohifadhi watoto nchini Syria yanatia shaka kwani mengi yao hayana ulinzi huku wengine wakilazimika kujiingiza kwenye kazi ili kuzisaidia familia zao.Kwa mujibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa, baadhi ya watoto wa kike wanaolewa wakiwa katika umri mdogo na wengine wanachukuliwa na kuingizwa kwenye makambi ya kijeshi na kugeuzwa wapiganaji.

Mashirika hayo lile la kuhudumia watoto UNICEF na lile linalohusika na wakimbizi UNHCR yameanzisha juhudi za kutambua matatizo hayo ili hatimaye kuyatafutia ufumbuzi.

Kwa upande wake UNHCR imesema kuwa inafanya kila liwezekanalo ili kuhakikisha kwamba wanawake wajawazito wanafikiwa na huduma bora za kiafya wakati wa kujifungua.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031