UNHCR yashutumu mauaji ya raia huko Mashariki mwa DRC,

Kusikiliza /

Wakimbizi wa DRC

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limeungana na mashirika mengine  ya Umoja huo kushutumu mauaji ya raia mwishoni mwa wiki wakati wa mapigano kati ya jeshi la serikali na waasi wa kundi la M23 huko Goma, mji mkuu wa Jimbo la Kivu Kaskazini. Alice Kariuki na maelezo zaidi.

(TAARIFA YA ALICE KARIUKI)

Mauwaji hayo yanafuatia mapigano makali yaliyoripotiwa kuzuka kaskazini mwa jimbo la Kivu, ambayo pia yamesabisha watu kadhaa kujeruhiwa.

Mji wa Goma ambao ni mji mkuu wa jimbohilo, unakusanya idadi kubwa ya raia waliokimbia mapigano yaliyozuka tangu mwaka jana.Adrian Edwards ni msemaji wa UNHCR

(Sauti ya Adrian Edwards)

Kiasi cha watu watatu waliuwawa na wengine watano wakijeruhiwa wakati kulipotokea mlipuko siku ya jumamosi asubuhi katika eneo la Ndosho nje kidogo ya mji wa Goma. Mlipuko mwingine ulizuka siku hiyo hiyo katika eneo lililopo karibu na kambi Magungu ambayo inahifadhi zaidi ya watu 14,000 waliokosa makazi. Tunazitolea wito pande zote kwenye mapigano hayo kujiweka kando na mashambulizi dhidi ya raia. Raia hawapaswi kulengwa.”

Katika hatua nyingine,UNHCR imesema kuwa wakimbizi kadhaa wanaokimbia mapigano katika jimbo la Kivu Kusin wameanza kumimini nchiniBurundi.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031