UM wakumbuka waliopoteza maisha wakisaidia wengine

Kusikiliza /

Kumbukumbu ya watumishi, UM

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya usaidizi wa kibinadamu Umoja wa Mataifa umefanya kumbukumbu ya watumishi wake waliopoteza maisha wakiokoa maisha ya wengine. Assumpta Massoi na taarifa zaidi.

(Taarifa ya Assumpta)

Kumbukumbu hiyo ya wafanyakazi 30 waliokufa kati ya Septemba mwaka jana na Juni mwaka huu imeandaliwa na Katibu Mkuu Ban Ki-Moon na imetilia maanani pia watumishi 22 wa umoja huo waliouawa huko Baghdad, Iraq miaka Kumi iliyopita ambapo shughuli ilihusisha uwekaji shada la maua, kuwasha mshumaa maalum na dakika moja ya ukimya.

Na ndipo Katibu Mkuu akahutubia akisema kuwa mashambulio dhidi ya wafanyakazi wa Umoja wa mataifa yanakatisha maisha ya watu walio mstari wa mbele kuokoa maisha yaw engine, akagusia pia watendaji wengine wakiwemo waandishi wa habari. Bwana Ban akasema Umoja wa Mataifa uko macho lakini kuna changamoto…

(Sauti ya Ban Ki-Moon)

"Japo tunajaribu kuimarisha utayari wetu na kuchukua hatua dhidi ya wanaotushambulia, wale wanaotulenga wameimarika sana na wana silaha za hali ya juu. Tumejifunza kutokana na waliopoteza maisha, naa tunabadili mwenendo wa operesheni zetu kote duniani. Wenzetu wamepoteza maisha, lakini moyo wao wa kusaidia wengine utaendelea katika tukio la leo na mwaka mzima. Tutakuwa tumetoa kumbukumbu muhimu kabisa kwao kwa kuendeleza kazi zao."

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031