Ulemavu siyo sababu ya kushindwa kujishugulisha,mkimbizi atoa mwanga wa matumaini

Kusikiliza /

Adam Mugisho

Raia mmoja aliyekimbia mapigano katika Jamhuri ya Demokrasia ya Congo na kuanzisha maisha ya ukimbizi katika nchi jirani yaUganda, ametuma ujumbe wa matumaini kwa kuanzisha ujasiliamali akishirikiana na wenzie kumi ikiwa ni muda mchache tu baada ya kuingia katika nchi ya uhamishoni.Adam Mugisho ambaye ni mlemavu wa miguu kutokana na tatizo la polio, amefungua duka dogo lililopo chini ya mti na anaendesha shughuli za utengenezaji wa simu za mikononi na radio ambazo zililetwa nchini humo na wakimbizi wenzake.

Historia ya kijana huyo inaonyesha alianza kujishughuli tangu akiwa nchiniCongoambako alifanya kazi kushona viatu huku wazazi wake wakimwacha bila kumpa matumaini. Anasema kuwa hali hiyo haikumvunja moyo badala yake alijipa matumaini yeye mwenyewe.

Marafiki wake wa karibu wamesema kuwa muda mfupi baada ya kuwasili katika kambi ya Bubukwanga iliyoko umbali wa kilometa 25 kutoka mpaka wa Congo kijana huyo ndiye alikuwa mkimbizi wa kwanza kuanzisha duka.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031