Takriban watu 150,000 waathiriwa na mafuriko nchini Sudan

Kusikiliza /

Athari za mafuriko nchini Sudan

Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchiniSudanimesema ina wasiwasi na mafuriko yanayoendelea kushuhudiwa kwenye majimbo manane nchini Sudan kufuatia mvua kubwa ambazo zimenyesha kuanzia mapema mwezi huu. Assumpta Massoi na taarifa kamili.

(RIPOTI YA ASSUMPTA MASSOI)

Zaidi ya watu 150,000 tayari wameathiriwa na mafuriko  hayo nchini Sudan, hiyo ni kwa mujibu wa mashirika kadha likiwepo la mwezi mwekundu nchini Sudan, Tume inayohusika na huduma za kibinadamu nchini Sudan, pamoja na Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM. Mvua zaidi zinatarajiwa siku zinazokuja huku idadi ya wale ambao wataathiriwa nao ikitarajiwa kuongezeka . Kiwango cha uharibifu kutokana na mafuriko hayo hakijulikani hadi sasa lakini makadirio ya hivi punde yanaonyesha kuwa nyumba Elfu 26 zimeharibiwa. Mashirilka ya Umoja wa Mataifa na washirika wao  wanafanya kazi kwa pamoja kukadiria mahitaji ili waweze msaada kwenye maeneo yaliyoathirika zaidi na mafuriko hayo wakati mahitaji ya sasa yakiwa ni chakula, makazi, maji na usafi na huduma za afya.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031