Sri Lanka inaelekea kwenye utawala wa kimabavu:Pillay

Kusikiliza /

Navi Pillay

Kamishna mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay leo amesema ingawa vita vimeishaSri Lanka, mateso bado yapo. Ameyasema hayo wakati akihitimisha ziara ya wiki moja nchini humo ambako ameonya kwamba tifa hilo la Asia linapanda mbegu ya hatma ambayo itaghubikwa na ukosefu wa uhuru wa kutosha na haki za binadamu.Akizungumza na waandishi habari mjini Colombo Bi Pillay amesema anasikitishwa na Sri Lanka kwamba licha ya fursa iliyokuwa nayo ya kumalizika kwa vita  kujenga taifa lenye mtazammo mpya sasa inaelekea kwenye utawala wa kimabavu. Amesema ni muhimu kila mmoja akatambua kwamba ingawa vita vimekwisha mateso hayajesha, akiongeza kuwa ingawa serikali imepiga hatua kwa msaada wa nchi wahisani , mashirika ya Umoja wa Mataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali , ujensi mpya pekee hauwezi kuleta maridhiano, utu au amani ya kudumu. Amesema mtazamo thabiti unahitajika ili kuleta ukweli, haki na maridhiano kwa watu waliathirika wakati wa vita. Ameonya dhidi ya kutowpa watu uhuru na haki za binadamu ,ukwepaji wa sheria na utawala wa sheria. Wakati wa ziara yake Bi Pillay amekutana na Rais Mahinda Rajapaksa na viongozi wengine wa serikali na kuwa na mazungu8mzo na maafisa wa mfumo wa sheria , wajumbe wa tume ya kitaifa ya haki za binadamu na kamati maalumu ya mapendekeo ya somo lililopatikana wakati wa vita.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031