Pongezi Mali kwa kuhitimisha mchakato wa uchaguzi wa Rais:Prod

Kusikiliza /

Romano Prodi

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye eneo la Sahel bwana Romano Prodi, amewapongeza watu wa Mali na Rais mchaguliwa Ibrahim Boubacar Keita kwa kuhitimisha vyema mchakato wa uchaguzi.

Bwana Prodi amempongeza pia mgombea urais aliyeshika nafasi ya pili bwana Soumaïla Cissé, kwa ushiriki wake muhimu kwenye mchakato huo wa uchaguzi. Hitimisho la uchaguzi wa Rais ni hatua kubwa katika kurejesha amani na demokrasia Mali. Na mafanikio ya mchakato huo yatachangia zaidi kuimarisha mfumo wa demokrasia ambao utaisaidia Mali kuwa na mustakhbali mzuri siku za usoni.

Bwana Prodi amesema sasa mtazamo uelekezwe katika kuimarisha taasisi za kidemokrasia, kukumbatia maridhiano ya kitaifa na kuchagiza maendeleo kwa kukuza uchumi na kuunda fursa za kazi.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031