Pillay ataka madai ya kuuawa kwa wanajeshi wa Syria kufanyiwa uchunguzi

Kusikiliza /

Navi Pillay

Kamishina mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema kuwa madai kuwa makundi ya upinzani nchini Syria yaliwaua wanajeshi wa serikali waliokamtwa wakati wa mapigano eneo la Khan Al-Assal mwezi uliopita ni ya kushangaza. Alice kariuki na taarifa kamili

(TAARIFA YA ALICE KARIUKI)

Picha za video zilizonaswa na vikosi vya upinzani eneo la Khan Al- Assal ziliwekwa kwenye mtandao kati ya tarehe 22 na 26 mwezi Julai. Kanda moja ya video inaonyesha wanajeshi wa serikali wakiamrishwa kulala chini huku nyingine ikionyesha miili ikitabakaa na mingine ikiwa pembeni. Pillay amesema kuwa ikiwa picha hizi zitathibitishwa zitaonyesha kuwa mauaji yalitendeka eneo la Khan Al-Assal. Amesema kuwa uchunguzi huru unahitajika kufanywa kubaini iwapo uhalifu wa kivita umetendeka ili wale wote waliohusika waweze kufikishwa mbele ya sheria. Pillay amesema kuwa kundi lake katika eneo hilo linaendesha uchunguzi ambapo limekagua kanda hizo na kuwahoji watu kwenye mji wa Aleppo. Ukanda wa kwanza unaonyesja watu wawili wasio na sare waliokuwa hai awali ambao walionekana wamekufa kwenye ukanda wa pili.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031